FREEMAN Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), anawindwa jimboni kwake Hai, Kilimanjaro. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).
Mwita Waitara, Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), amemwelekeza Lengai Ole Sabaya, Mkuu wa Wilaya ya Hai kufuata fedha za mfuko wa Jimbo la Hai na kupanga matumizi.
Amesema, fedha hizo Sh. 42 milioni zipo kwa Mbowe tangu mwaka 2018/19 na hazijapangiwa matumizi, na sasa miaka miwili imepita bila kutumika.
Akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai, tarehe 8 Januari 2020, Waitara amesema, mwenye mamlaka ya kupanga matumizi ya fedha hizo si Mbowe bali ni Mkuu wa Wilaya na mkurugenzi.
Mwita amemtaka Sabaya kumwagiza mkurugenzi wa halmashauri hiyo kufanya utaratibu wa kupata fedha na kupanga matumizi yake naye (Sabaya) kusimamia.
Pia amemtuhumu Mbowe ambaye ni Mbunge wa Hai, kwamba amekuwa mtoro na hafanyi kazi za jimbo, na amekuwa akifanya matumizi ya fedha hizo kwa njia ya simu, kitu ambacho hakikubaliki.
MwanaHALISI Online leo tarehe 9 Januari 2020, limemtafuta Mbowe ili kupata ufafanuzi kuhusu tuhuma hizo bila mafanikio. Na hata alipoandikiwa ujumbe mfupi wa maneno, hajajibu.
Kwenye mkutano huo, Sabaya amemuahidi Mwita kwamba, hakuna fedha zitazochezewa na kwamba, yoyote atakayejaribu kufanya hivyo, atamfyatua.
Leave a comment