Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mtoto wa miaka mitano afariki kwa moto
Habari Mchanganyiko

Mtoto wa miaka mitano afariki kwa moto

Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, ACP Jonathan Shanna
Spread the love

MTOTO wa miaka mitano, Solile Emannuel amefariki dunia katika ajali ya moto iliyotokea tarehe 3 Oktoba 2018 nyumbani kwao maeneo ya Nh’obola wilayani Nayamaga mkoa wa Mwanza. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza kuhusu tukio hilo leo tarehe 6 Oktoba 2018, Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, ACP Jonathan Shanna amesema chanzo cha moto huo ni kuungua kwa godoro kulikosababishwa na marehemu alipokuwa anachezea njiti ya kiberiti.

Kamanda Shanna ameeleza kuwa, wakati mtoto huyo anafanya tukio hilo, aliachwa peke yake na wazazi wake waliokuwa bustanini wakilima.

“Tukio hilo limetokea tarehe 3 saa 17:00 jioni, wakati marehemu alipoachwa peke yake chumbani akila chakula huku wazazi wake wakiwa bustanini wakilima. Inadaiwa marehemu alikuwa akichezea njiti ya kiberiti na kupelekea kuwasha moto ulioanza kuunguza godoro, nguo na hatimaye kushika nyumba nzima hali iliyopelekea marehemu kukosa hewa na baadae kufariki dunia,” ameeleza Kamanda Shanna.

Amesema, baada ya tukio hilo kutokea, Jeshi la Polisi lilifika kwa haraka eneo la tukio na kushirkiana na wananchi kutoa msaada, lakini moto ulikuwa tayari umepoteza uhai wa mtoto na kutekeza mali na vitu vyote katika nyumba hiiyo.

“Thamani ya mali na vitu vilivyoteketea katika ajali hiyo bado haijafahamika. Mwili wa marehemu tayari umefanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya mazishi,” amesema.

Kufuatia tukio hilo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, limewasisitiza wazazi na walezi kuwa waangalifu na watoto wakati wote, na waache tabia ya kuwaacha watoto kwenye nyumba peke yao kwani kunaweza kuhatarisha usalama wao na baadae kupata majeruhi au kufariki dunia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!