March 9, 2021

Uhuru hauna Mipaka

China yashukiwa kupotea kwa Rais wa Interpol

Rais wa Shirika la Polisi la Kimataifa (Interpol), Meng Hongwei

Spread the love

UTATA umeibuka kufuatia madai ya kupotea kwa Rais wa Shirika la Polisi la Kimataifa (Interpol), Meng Hongwei baada ya  Afisa Mkuu wa masuala ya sheria nchini Ufaransa kukana kwamba kiongozi huyo hakuwa nchini humo wakati alipopotea. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Wakati hayo yakijiri kwa mujibu wa gazeti la South China Morning Post  la Hong Kong, liliripoti kuwa Hongwei  yuko ndani ya uchunguzi nchini humo kwa sababu zisizojulikana, huku likiadai kwamba, Mkuu huyo wa Interpol ambaye aliwahi kuwa naibu waziri wa usalama wa umma China alichukuliwa na vyombo vya dola kwa ajili ya kuhojiwa mara tu alipowasili nchini humo.

Hata hivyo, Msemaji wa Interpol aliyekataa kutaja jina lake, aligoma kusema kama Hongwei alikwenda China kwa kazi maalum. Taarifa zinadai kuwa Hongwei alikwenda nchini humo kuichokonoa Beijing.

Katika hatua nyingine, Wizara ya Mambo ya Ndani nchini Ufaransa hapo jana ilitoa ripoti ya kwamba, mke wa Hongwei alikwenda katika makao makuu ya Interpol yaliyoko mjini Lyon nchini humo, kuripoti taarifa za kupotea kwa mume wake.

Taarifa ya wizara hiyo, ilieleza kuwa, Ufaransa inafanya uchunguzi wa tukio hilo ambapo imefungua jalada la uchunguzi,  vile vile  linafuatilia vitisho anavyopokea mke wa rais huyo, sambamba na polisi wake kutumia mbinu za hali ya juu kuhakikisha mwanamama huyo anakuwa salama.

error: Content is protected !!