Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mtatiro awajibu waliomvua uanachama
Habari za SiasaTangulizi

Mtatiro awajibu waliomvua uanachama

Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa chama cha CUF, Julias Mtatiro akizungumza na waandishi wa habari
Spread the love

MWENYEKITI wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Wananchi (CUF), Julius Mtatiro amejibu uongozi wa CUF wilaya ya Ubungo, uliomvua uanachama, na kusema kuwa hatajishughulisha na tangazo hilo na siyo jipya kwake, yeye anaendelea na majukumu yake kama kawaida. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Mtatiro ameandika katika ukurasa wake wa Facebook, kuwa hiyo siyo mara ya kwanza kwa kikundi hicho alichokiita cha kihuni kutangaza kumvua uanachama, hivyo hawawezi kumshughulisha wala kuwashughulisha wenzake wanaofanya majukumu yao kitaifa.

Katika waraka huo wa Mtatiro amesema anawasubiri wahuni hao watangaze kumfukuza mara ya tatu, ya nne, ya tano na ya sita, lakini hatashtuka. Soma zaidi walaka huo hapa chini.

Ndugu zangu.

Nimeona taarifa kwenye mitandao kuwa kuna watu wanajiita viongozi wa CUF wilaya ya Ubungo na kwamba ati wamenivua uanachama wa CUF.

Bila shaka hawa ni vijana wa Bwana Yule na wanatumika kututoa kwenye ajenda kubwa za kitaifa. Mwezi Disemba mwaka jana pia wahuni hao walitangaza ati wamenivua uanachama, tangazo lao la jana si jipya!

Mimi naendelea na majukumu yangu kama Kiongozi wa Juu wa chama anayetambuliwa na chama na vikao vya chama, na vitangazo hivyo vya wahuni haviwezi kunishughulisha wala kuwashughulisha wenzangu.

Nasubiri tangazo lingine la wahuni hao, la kunifukuza uanachama mara ya 3, ya 4, ya 5 na ya 6.

Hawatushughulishi kabisa maana dawa ya mgonjwa ni kumpa dawa tu.

Mtatiro J,
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi Taifa,
The Civic United Front (CUF),
05 Machi 2018.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!