May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mshambuliaji Dodoma jiji ashinda tuzo

Spread the love

 

ANWARI Jabir, mshambuliaji wa Dodoma Jiji, ameshinda tuzo ya mchezaji bora mwezi Februari 2021, kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mshambuliaji huyo, amechukua tuzo hiyo mara baada ya kuwashinda mshambuliaji wa KMC, Charles Ilanfya na Issa Ngoah wa Dodoma Jiji.

Ndani ya mwezi Februari, Anwari aliisaidia timu yake ya Dodoma Jiji kushinda michezo mitano na kutoka sare mmoja huku akiweka kambani mabao manne.

Kwa sasa Dodoma Jiji iko nafasi ya tano ya msimamo ikiwa na pointi 32.

Anwari anakuwa mchezaji wa tano kutwaa tuzo hiyo toka mwezi Septemba 2020, wakati Ligi hiyo inaanza.

Wachezaji wengine ambao tayari wameshatwaa tuzo hiyo ni Price Dube (Septemba-Azam), Mukoko Tonombe (Oktoba- Yanga), John Bocco (Novemba- Simba), Saido Ntibanzokiza (Desemba- Yanga) na Deogratius Mafie (Januari-Biashara United).

error: Content is protected !!