May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Katwila awabwaga Makata, Simkoko tuzo VPL

Spread the love

 

KOCHA wa kikosi cha Ihefu FC ya Mbeya, Zuber Katwila ameshinda tuzo ya kocha bora mwezi Februari 2021, kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Katwilwa, ametwaa tuzo hiyo, mara baada ya kuwashinda Mbwana Makata wa KMC ya Kinondoni, Dar es Salaam na John Simkoko wa Dodoma Jiji.

Ndani ya Februari, Katwila aliongoza Ihefu kwenye michezo mitatu na kufanikiwa kuibuka na ushindi kwenye mechi mbili na kwenda sare mara moja.

Kwa matokeo hayo, yalitosha kumfanya Katwila kuitoa timu hiyo kwenye nafasi ya 18 kwenye msimamo hadi nafasi ya 16, ikiwa na pointi 20.

Katwila ambaye amejiunga na timu hiyo kutokea Mtibwa Sugar, ametwaa tuzo hiyo kwa mara ya kwanza toka kuanza kwa msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2020/21.

Makocha wengine walioshinia tuzo hiyo toka kuanza kwa msimu huu ni Aristica Cioaba aliyekuwa kocha wa Azam FC kwa mwezi Septemba, Cedric Kaze, alifanikiwa kutwaa tuzo hiyo mwezi Oktoba, Charles Mkwasa alijinyakulia tuzo hiyo akiwa na kikosi cha Ruvu Shooting mwezi Novemba.

Pia, Cedric Kaze alitwaa tena tuzo hiyo mwezi Desemba na kisha Kocha wa Biashara United, Francis Baraza alichukua tuzo hiyo Januari.

error: Content is protected !!