Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Msako wa kuwakamata waganga wa kienyeji watangazwa
Habari Mchanganyiko

Msako wa kuwakamata waganga wa kienyeji watangazwa

Sehemu ya vifaa vya waganga wapiga ramli
Spread the love

JESHI la Polisi nchini limetangaza msako wa kuwakamata na kuwadhibiti waganga wa tiba asili wanaojihusisha na vitendo vya upigaji wa ramli chonganishi zinazochangia kuwepo kwa mauaji ya watu hapa nchini. Anaripoti Moses Mseti, Magu … (endelea).

Msako huo umetangazwa ikiwa ni siku chache tangu kutokea kwa mauaji ya watoto wadogo na vikongwe katika mikoa ya Njombe na Simiyu yanayohusishwa na imani potovu za kishirikina 

Msako huo umetangazwa leo na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro wakati akizungumza na kamati ya ulinzi na usalama na askari Polisi wa Wilaya za Magu na Kwimba mkoani Mwanza ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kikazi katika mikoa ya kanda ya ziwa.

IGP Sirro, amesema jeshi la Polisi litaendelea kufanya misako ya mara jwa marao ili kuwabaini waganga wa tiba asili wanaofanya vitendo vya upigaji ramli chonganishi zinazosababisha kuendelea kuwepo kwa mauaji ya kutisha kwa raia, yanayotokana na imani potofu.

“Matatizo yaliopo simiyu (mkoa) hayana utofauti na Magu ni sawa kwa hiyo niwaonbe sana suala hili lazima tuwe na msako wa mara kwa mara na speed (kasi) ya hawa jamaa ni kubwa.

“Hawa jamaa wakiwa stable bila kuwa stabilize watatusumbua, muda wote ni kuwakamata ukiingia kwenye nyumba ya mganga wa kienyeji lazima utakuwa gorvement office (ofisi ya serikali) utakuta kuna mkia wa mende na vitu vingi,” amesema Sirro.

Amesema mipango ya jeshi hilo ni kuwasumbua waganga hao wasipate muda wa kutulia na kamata kamata hiyo itasaidia kupunguza tatizo la upigaji ramli chonganishi na vifo vitokanavyo na tatizo hilo.

Katika hatua nyingine IGP Sirro amewatama askari Polisi kuacha kujihusisha vitendo vya rushwa vinavyochangia kushusha heshima ya askari pamoja na kuwahimiza kupunguza vitendo vya uhalifu kwenye maeneo yao.

“Heshima yenu ni kupunguza uhalifu pamoja na rushwa na rushwa yenyewe ni shilingi elfu mbili na hizi ndogondogo, we have to change (lazima tubadilike).

“Askari akimuona mtu anakuja tu unafikiria pesa yake mfukoni utafikiri ulimsaidia kutafuta it’s going to cost you hii inaenda kukuumiza,” amesema Sirro.

Mkuu wa Wilaya ya Kwimba, Senyi Ngaga amesema katika kipindi cha Januari mpaka sasa kuna makosa 27 ya mimba za utotoni na kwamba pamoja na hilo bado kuna idadi kubwa ya watoto wanaobakwa.

“Ukiacha mimba za utotoni kuna watoto wengi ambao wanaobakwa kwa hiyo bado tunaendelea kuangalia sheria ichukue mkondo wake lakini inakuwa ni ngumu Sana,” amesema Ngaga.

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Kwimba, Shanif Mansoor amesema ongezeko kubwa la mimba za utotoni katika maeneo mengi nchini linachangiwa na ukosefu wa elimu, hivyo, amehimiza kuendelea kutolewa kwa elimu kwenye jamii pamoja na mabinti wadogo.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!