Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Sumaye apokea msaada wa Pikipiki
Habari za Siasa

Sumaye apokea msaada wa Pikipiki

Spread the love

CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), katika Kanda ya Pwani, kimekabidhiwa pikipiki nne kwa ajili ya kujiandaa na uchaguzi wa Serikali za Mitaa na uchaguzi mkuu wa mwaka 2020. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Akikabidhi Pikipiki hizo, Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Kinondoni, Suzana Lyimo, amesema kuwa vyombo hivyo amevitoa ili kusaidia shughuli za chama.

“Hizi Pikipiki nimezitoa kwa ajili ya ujenzi wa chama; na siyo venginevyo. Ni rai yangu kuwa watakaokabidhiwa Pikipiki hizi, wazifanyike kazi zilizokusudiwa,” alieleza.

Akizungumza mbele ya Frederick Sumaye, mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, mwenyekiti wa Kanda hiyo, Lyimo alisema, “Pikipiki ni mali ya chama. Ni lazima zitumike kwa ajili ya kazi hiyo.”

Alisema, “narudia kuwaomba sana, tena sana, wale watakaozitumia tofauti, kusiwe na kigugumizi cha kuwanyang’anya.”

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unatarajiwa kifanyika mapema mwaka huu.

Pikipiki ambazo Lyimo amezikabidhi zitatumika kwa ajili ya majimbo manne ya uchaguzi ya Ubungo, Kibamba, Kinodnoni na Kawe.

Naye Sumaye akipokea Pikipiki hizo, alimshukuru mbunge huyo na kuwataka wabunge wengine kuiga mfano wake.

Sumaye alimuahidi kuwa uongozi wake utahakikisha Pikipiki alizotoa zitatumika kwa ajili ya kazi za chama na kwa Kanda ya Pwani.

Wakati huo huo, Sumaye amemkabidhi Pikipiki hizo, John Mnyika, naibu katibu mkuu (Chadema Bara), ili kuainisha kuwa chama hicho kimepokea vyombo hivyo.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mnyika amesema, amepokea Pikipiki hizo kwa niaba ya chama na kusisitiza zitatumika kwa ajili ya uenezi wa chama kuanzia ngazi chini (nyumba kwa nyumba).

Naye mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea amesema, amefurahi kupokea vyombo hivyo na kumshukuru mbunge huyo wa Viti Maalum kwa mchango wake. Kubenea alitoa kauli hiyo kwa niaba ya wabunge wenzake.

Amesema, yeye na wabunge wenzake watahakikisha kazi iliyofanywa na mbunge Lyimo italindwa kwa gharama yoyote ile.

Amewataka viongozi wa majimbo mengine kuzikarabati pikipiki zilizokuwemo kwenye majimbo yao  ili zitumike kwa shughuli za chama.

Waziri Muhunzi, mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Kinondoni, alitoa neno la shukurani kwa niaba ya makatibu na wenyeviti wote majimbo yaliyopokea Pikipiki hizo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Serikali yawaangukia viongozi wa dini

Spread the loveSERIKALI imewaomba viongozi wa dini, waendelee kuelimisha wananchi kudumisha amani...

Habari za Siasa

Azzim Dewji aitaka Serikali iwanyooshe mafisadi

Spread the loveMFANYABIASHARA maarufu nchini, Azzim Dewji, ameitaka Serikali iwachukulie hatua wezi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari za Siasa

Mgongano wa kimasilahi wamhamisha Chande TTCL

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),...

error: Content is protected !!