Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mrithi wa Dk. Tulia kupatikana Februari 11
Habari za Siasa

Mrithi wa Dk. Tulia kupatikana Februari 11

Dk. Tulia Ackson, Spika wa Bunge la Tanzania
Spread the love

 

BUNGE la Tanzania limetanganza mchakato wa kujanza nafasi ya naibu spika wa Bunge ambapo uchaguzi wake utafanyika tarehe 11 Februari 2022. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Uchaguzi huo unafanyika kujaza nafasi hiyo iliyoachwa wazi na Dk. Tulia Ackson ambaye alijiuzulu tarehe 31 Januari 2022, baada ya kuteuliwa na chama chake- Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania uspika.

Dk. Tulia alikuwa miongoni mwa wagombea tisa waliojitokeza kugombea uspika Jumanne iliyopita ya tarehe 1 Februari 2022 na kushinda kwa kura zote za wabunge 376 waliopiga kura sawa na asilimia 100.

Dk. Tulia amechukua nafasi ya Job Ndugai ambaye tarehe 6 Januari 2022 alitangaza kujiuzulu.

Ndugai alichukua uamuzi huo baada ya kushinikizwa na viongozi wa CCM kutokana na kauli yake ya kukosoa mwenendo wa serikali kukoka fedha nje za kugharamikia miradi ya maendeleo kokosolewa vikali.

Leo Alhamisi, tarehe 3 Februari 2022, Ofisi ya Bunge imetoa taarifa kwa umma kikivitaarifu vyama vyenye uwakilishi bungeni kuweza kuanza mchakato wa kujaza nafasi hiyo.

“Chama kinachokusudia kushiriki uchaguzi, kinashauriwa kuanza mchakato wa kumpata mgombea kutoka miongoni mwa wabunge wa chama hicho,” imeeleza taaifa hiyo na kuongeza:

“Uchaguzi umepangwa kufanyika tarehe 11 Februari 2022. Hivyo jina la mgombea linapaswa kuwasilishwa kwa msimamizi wa uchaguzi kabla ya saa 10:00 jioni ya tarehe 10 Februari 2022, katika ofisi ya katibu wa Bunge.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo Dar wampa tano Rais Samia

Spread the love  NGOME ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo, kimempongeza Rais...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yaiangukia Serikali kunusuru wananchi Liwale, Nachingwea

Spread the love  CHAMA cha ACT-Wazalendo, kimeitaka Serikali kuchukua hatua za haraka...

Habari za SiasaTangulizi

Vigogo wanaokwamisha mradi Liganga na Mchuchuma kitanzani

Spread the love  NAIBU Spika wa Bunge, Mussa Zungu, watu wanaokwamisha utekelezaji...

Habari za Siasa

Gridi ya Taifa kufumuliwa kukabiliana na katizo la mgao wa umeme

Spread the love  WAZIRI wa Nishati, Januari Makamba, amesema Serikali ina mpango...

error: Content is protected !!