October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mpakistani kizimbani kwa rushwa  

Spread the love

MUHAMMEDI Hasnain Hyderi, Raia wa Pakistan amepandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Slaam kwa tuhuma za rushwa. Anaripoti Faki Sosi…(endelea). 

Leo Alhamisi tarehe 17 Januari 2019 kwenye mahakama hiyo mbele ya Hakimu Wanjah Hamza, Wakili wa Serikali Pascal  Magabi amemsomea shtaka moja Hydari la kutoa rushwa kwa Ofisa wa Mamlaka ya Mapato (TRA) ili asimdai kodi.

Wakili Pascal amedai kuwa, tarehe 15 Januari mwaka huu eneo la BestBite, jijini Dar es Salaam Hydari alimshawishi Ofisa wa TRA, Talib Abdul Kombo asimdai kodi kwa kutaka kumpa rushwa ya Sh. Mil 2.

Upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na mtuhumiwa  amekana shitka hilo. Mahakama imempa masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili wenye kutambuliwa na taasisi za serikali watakao saini bondi ya Shiling Milion 5 kila mmoja.

Pia raia huyo ametakiwa awasilishe hati ya kusafiria mahamakamani hapo. Hakimu Hamza ameahirisha kesi hiyo mpaka terehe 31 Januari mwaka huu.

error: Content is protected !!