October 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbowe mgonjwa, ashindwa kufika mahakamani

Baadhi ya Vigogo wa Chadema waliohudhuria mahakamani Kisutu leo

Spread the love

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, ni mgonjwa, hali iliyopelekea kushindwa kufika mahakamani. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Hayo yameelezwa leo Alhamisi, tarehe 17 Januari 2019, mbele ya Hakimu Mkazi Kisutu, Wilbrad Mashauri.

Wakili mkuu wa Serikali, Patrick Mwita, ameambia Mahakama kuwa Mbowe anaumwa na hivyo, “ameshindwa kufika mahakamani.”

Wakili Mwita amesema kuwa upande wa mashtaka umepata taarifa kutoka jeshi la Magereza kuwa mtuhumiwa huyo anaumwa na ndio sababu ya kutofika mahakamani.

Mbowe ambaye ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni pia Mbunge wa Hai na viongozi wengine wa chama hicho wanakabiliwa na tuhuma za kufanya maandamano na mikusanyiko kinyume na sheria.

Watuhumiwa wengine ni pamoja Dk. Vicent Mashinji, Katibu Mkuu wa Chadema; Jonh Mnyika, Naibu Katibu (Chadema) Bara; Salum Mwalim, Naibu Katibu (Chadema) Zanzibar; Halima Mdee, Mbunge wa Kawe; John Heche, Mbunge wa Tarime Mjini.

Wengine ni Ester Bulaya, Mbunge wa Bunda Mjini; Ester Matiko, Mbunge Tarime Vijijini na Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini.

Leo tarehe 17 Januari 2019 Wakili wa Serikali Patrick Mwita mbele ya Hakimu Mkazi Wilbard Mashauri ameieleza mahakama kuwa, upande wa mashtaka umepata taarifa kutoka Magereza kuwa mtuhumiwa namba moja (Mbowe) anaumwa ndio sababu ya kutofika mahakamani hapo.

Mwita ameeleza kuwa, kesi hiyo imefika kwa ajili ya kutajwa kwenye mahakama hiyo (Kisutu) na kwamba, mpaka rufaa ya dhamana itakapomalika. Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo mpaka tarehe 31 Januari mwaka huu.

 

error: Content is protected !!