July 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mourinho aingia kwenye rekodi mpya barani Ulaya

Spread the love

 

KOCHA wa zamani wa Chelsea na Manchester United za Uingereza, Jose Mourinho ambaye kwa sasa anakinoa kikosi cha AS Roma ameimeingia kwenye rekodi mpya barani ulaya kwa kuwa kocha wa pili kushinda mataji mengi Barani Ulaya. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mourinho ameingia kwenye rekodi hiyo, kufuatia siku ya jana tarehe 25 Mei 2022, alikiongoza kikosi cha AS Roma kutwaa taji la ulaya (UEFA Conference League), mara baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 1-0, kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Fayenoord.

Taji hilo linamfanya kocha huyo kushinda taji la tano barani humo, katika historia yake ya soka toka alipotwaa taji la kwanza la Ligi ya Mabingwa akiwa na FC Porto.

Mataji ambayo mpaka sasa Mourinho ameyashinda barani humo akiwa katika klabu tofauti ni Ligi ya Mabingwa barani humo mara mbili akiwa na klabu za FC Porto na Intermilan, UEFA Europa Ligi na Super Cup.

Rekodi hiyo inamfanya Mourinho kushika nafasi ya pili kwa kuwa kocha mwenye mataji mengi barani Ulaya, nyuma ya Giovanni Trapattoni kocha Raia wa Italy ambaye alizinoa klabu za Fiorentina na Bayern Munchen anayeshiklia rekodi ya kutwa mataji ya Barani Ulaya mara tano.

Licha ya kutwaa taji hilo, Mourinho ameonekana kutokuwa na nia ya kuondoa kwenye klabu hiyo, ambayo alijiunga nayo akitokea Tottenham ya nchini Uingereza.

error: Content is protected !!