August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bosi DAWASA ateuliwa NARCO

Mhandisi Cyprian Luhemeja

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Mhandisi Cyprian Luhemeja kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Utuuzi huo umetanagwa usiku wa jana Jumatano tarehe 25 Mei 2022 na Zuhura Yunus, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu akiwa Accra nchini Ghana ambako Rais Samia yuko huko kwa ziara ya kikazi ya siku tatu inayomalizika leo Alhamisi.

Mhandisi Luhemeja ni Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA).

Aidha, Rais Samia alimteua Macrise Mbodo kuwa Postmasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC).

Kabla ya uteuzi huo, Mbondo alikuwa Kaimu Postmasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC).

error: Content is protected !!