Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Moto soko la K’koo: Rais Samia atoa pole, maagizo
Habari MchanganyikoTangulizi

Moto soko la K’koo: Rais Samia atoa pole, maagizo

Soko la Kariakoo likiwaka moto
Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ametoa pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla na wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo, kufuatia hasara kubwa waliyoipata kutokana na kuungua moto kwa soko hilo lililopo jijini humo. Anaripoti Ibrahim Yamola, Dar es Salaam … (endelea).

Moto ulioibuka jana usiku Jumamosi, umeteketeza soko hilo upande wa juu huku chini (shimoni) kukiwa hakujaathirika na moto huo ambao tayari vikosi vya ulinzi na usalama, vimekwisha kuuzima.

Leo Jumapili, tarehe 11 Julai 2021, taarifa iliyotolewa na Jaffar Haniu, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, imeeleza kuwa, Rais Samia ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi wa kina kujua chanzo cha moto huo.

Soma zaidi:-

Majaliwa akagua moto soko la Kariakoo, atoa siku saba

Rais Samia, amesema Soko Kuu la Kariakoo ni soko kubwa jijini Dar es salaam ambalo lina mkusanyiko mkubwa wa wafanyabiashara na kuteketea kwa soko hilo kutakuwa kumesababisha hasara kubwa kwa wapangaji na wamiliki wa soko hilo kongwe nchini.

Amesema Soko la Kariakoo licha ya kuajiri wafanyabiashara wengi lakini ni kitovu cha biashara kwa nchi za Afrika Mashariki hivyo tukio hilo si hasara kwa wafanyabiashara tu bali hata kwa Serikali.

Mapema leo asubuhi Jumapili, Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ametembelea soko hilo na kutoa siku saba kwa za awali kamati aliyoiunda kuchunguza chanzo cha moto katika soko hilo ili kubaini nini kimesababisha au nani kasababisha moto huo.

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Kamati iliyoundwa ambayo itafanya kazi na kamati ya ulinzi na usalama iliyoanza kufanya kazi chini ya Mkuu wa Mkoa huo itajumuisha Ofisi ya Rais-Ikulu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Ofisi ya Waziri Mkuu ambayo itawakilishwa na Mkurugenzi wa Maafa.

Wengine ni Vyombo vya Ulinzi na Usalama ikujumuisha Jeshi la Wananchi, Jeshi la Polisi, Zimamoto pamoja na Taasisi ya Kupambana na Rushwa.

Pia, Waziri Mkuu alizitaja Wakala wa Majengo, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Watendaji Kata, Mitaa watakaoshindwa kusimamia usafi kukiona

Spread the love  WATENDAJI wa kata, mitaa na vitongoji na maofisa afya...

Habari Mchanganyiko

Mtia nia urais TLS kukata rufaa kupinga kuenguliwa

Spread the love  MTIA nia ya kugombea Urais wa Chama cha Mawakili...

Habari Mchanganyiko

NBC yazindua kampeni ya mkeka wa ushindi na ATM zake

Spread the loveBENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imetangaza uzinduzi wa kampeni...

Habari Mchanganyiko

Uholanzi wampongeza Rais Samia kuimarisha vyombo vya habari, demokrasia

Spread the love  UBALOZI wa Uholanzi nchini Tanzania, umempongeza Rais Samia Suluhu...

error: Content is protected !!