May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia aagiza uchunguzi moto shule za dini

Bweni la Shule ya Sekondari ya Kiislam ya Wasichana AT TOWN likiteketea kwa moto

Spread the love

 

SAMIA Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kwa kushirikiana na Jumuiya za Kiislamu Tanzania kutafuta chanzo cha matukio ya moto yanayojitokeza kwenye shule zinazomilikiwa na Waislamu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Rais Samia ametoa maagizo hayo, leo Jumapili tarehe 11 Julai 2021, ikiwa ni siku moja imepita tangu moto ambao haujajulikana chanzo chake, kuteketeza Bweni la Shule ya Sekondari ya Kiislam ya Wasichana AT TOWN, iliyopo mji mpya, mkoani Morogoro.

Moto huo, uliibuka jana usiku Jumamosi, umetekeleza mara mbalimbali kama vitanda, magodoro, madaftari na vitabu.

Soma zaidi:-

Moto soko la Kariakoo, Rais Samia atoa pole, maagizo

Taarifa ya Jaffar Haniu, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, imemnukuu Rais Samia akitoa pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Martin Shigella na Jumuiya za Kiislaam Tanzania kufuatia kuungua moto kwa Bweni hilo.

Rais Samia amesema kumekuwa na matukio ya mara kwa mara ya kuungua moto kwa shule zinazomilikiwa na Jumuiya za dini nchini.

Kutokana na hilo, Rais Samia ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kwa kushirikiana na Jumuiya hizo kutafuta vyanzo vya matukio hayo na kuyadhibiti ili matukio ya kuungua moto kwa shule hizo yasijirudie.

error: Content is protected !!