May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Morrison ateka Show ya Simba Dar

Spread the love

 

DAKIKA tatu zilizotosha kumfanya Bernard Morisson kuibuka mchezaji bora wa mechi mara baada ya kupachika mabao mawili kwenye mchezo wa Kombe la Simba dhidi ya Al Hilal ya Sudan. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea)

Mchezo huo wa kujipima nguvu kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya Ligi ya mabingwa ambapo Simba walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-1.

Morrison ambaye aliingia dakika ya 62 ya kipindi cha pili akichukua nafasi ya Francis Kahata ambapo ilimchukua dakika 25 akiwa uwanjani kupachika bao lake la kwanza dakika ya 87, na dakika tatu baadae akapicha bao la pili ambalo lilikuwa bao la nne kwenye mchezo huo dakika ya 90.

Morrison hakuonekana uwanjani muda mrefu kutokana na kusumbuliwa na majeraha toka mwezi wa 12 mwaka jana.

 

Mara baada ya mchezo huo kocha mkuu wa klabu ya Simba, Didier Gomes alimuelezea mchezaji huyo kuwa anakipaji cha hali ya juu ila anahitaji kuwa fiti ili aweze kucheza mara kwa mara.

“Morrison ni mchezaji mzuri anahitaji kucheza muda mrefu, ameonesha kiwango kizuri anahitaji kuwa fiti kwa utimamu wa mwili kwa kuwa ni kitu muhimu” alisema Gomes.

Baada ya kupata matokeo hayo Simba itashuka tena dimbani siku ya Jumapili ambapo watavaana na TP Mazembe kwenye mchezo wa pili wamichuano hiyo.

error: Content is protected !!