August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mnyika amvaa Rais Magufuli, akosoa majadiliano

John Mnyika, Mbunge wa Jimbo la KIbamba

Spread the love

JOHN Mnyika, Waziri Kivuli wa Nishati na Madini amesema Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi hakustahili kuongoza timu ya inayoangalia masuala mbalimbali kuhusu mikataba ya madini hapa nchini, anaandika Hamisi Mguta.

Amesema kazi hiyo ingetakiwa kufanywa na  Waziri wa Nishati na Madini kwa kuwa yeye ndiyo mhusika katika sekta hiyo.

Mnyika ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kibamba ametoa hoja hiyo katika mkutano wake na wananchi wa jimbo hilo eneo la Goba mwisho.

Mazungumzo hayo yanafanyika jijini Dar es Salaam kati ya timu ya watalaam wa Tanzania na wenzao kutoka kampuni ya uchimbaji madini ya Barrick Gold Corporation.

“Kwanini mpaka leo Rais Magufuli hajateua Waziri wa Nishati na Madini ili aongoze majadiliano, anamchukua Waziri wa Katiba na sheria,” amehoji

Tazama VIDEO nzima hapo chini alichozungumza Mnyika…..

error: Content is protected !!