November 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mlipuko mpya corona, Uingereza yatengwa

Spread the love

NCHI ya Uingereza imetengwa na mataifa kadhaa ya Ulaya na Amerika kutokana na mlipuko mpya wa virusi vya corona. Inaripoti mitandao ya kimataifa…(endelea).

Mataifa hayo yakiwemo Argentina, Chile, Colombia na Canada, yamezuia abiria na treni zinazotoka Uingereza kuingia kwenye mataifa yao kuhofia maambukizi mapya kwenye mataifa yao.

Uamuzi wa mataifa hayo ulifikiwa saa chache baada ya Boris Johnson, Waziri Mkuu wa Uingereza kupiga marufuku mikusanyiko kwenye sherehe za Krismas Ijumaa wiki hii.

Waziri huyo amewaeleza Waingereza kwamba, sasa hawana budi kuhakikisha wanafuata kikamilifu taratibu za kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona.

Mataifa ya France, Ujerumani, Uholanzi, Italia, Ubelgiji, Australia, Ireland and Bulgaria ndio yaliyotangulia kupiga marufuku wageni kutoka Uingereza.

Tayari Waziri wa Afya wa Uingereza, Matt Hancock jana tarehe 20 Desemba 2020, alitangaza sheria kali ili kukabiliana na maambukizi hayo mapya.

error: Content is protected !!