Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mkurugenzi TPDC, wenzake wafutiwa kesi
Habari Mchanganyiko

Mkurugenzi TPDC, wenzake wafutiwa kesi

James Mataragio, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petrol (TPDC)
Spread the love

JAMES Mataragio, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petrol (TPDC), ameachwa huru na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo tarehe 19 Agosti 2019. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Hatua hiyo imetokana na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), kutokuwa na nia ya kuendelea na mashitaka dhidi ya Mataragio na wenzake.

Mataragio alipandishwa kizimbani kwa tuhuma ya matumizi mabaya ya madaraka. Baada ya kuwa nje ya ofisi kwa miaka mitatu sasa, mkurugenzi huyo amerejeshwa kazini.

Hatua ya kuachwa huru Mataragio ilitanguliwa na agizo la Rais John Magufuli kwamba, ofisa huyo arejeshwe kwenye nafasi yake.

Kwenye tuhuma hizo, washtakiwa wengine walioachiwa ni pamoja na Edwin Riwa , aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Mipango,  Welington Hudson, aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi na Utawala na Kelvin Komba, aliyekuwa Mkurugenzi wa Mkondo wa Juu.

Kelvin Mhina, Hakimu Mkazi Mfawidhi amewafutia mashitaka hayo baada ya DPP kupitia Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon kuwasilisha ombo la kusitisha kesi hiyo tangu tarehe 10 Julai 2019.

DPP amesitisha kesi hiyo kwa kutumia kifungu cha 91 (1) cha Sheria ya Makosa ya Jinai (CPA) Sura ya 20 ambapo, Hakimu Mhina aliwaachia huru kwa kutumia sheria hiyo.

Mataragio na wenzake walidaiwa kati ya Aprili 8, 2015 na Juni 3, 2016, wakiwa watumishi wa umma (TPDC) kwa nafasi zao, walitumia madaraka vibaya.

Pia walituhumiwa kubadilisha na kupitisha bajeti na mpango wa ununuzi wa mwaka 2014/2015 na 2015/2016 kwa kuingiza ununuzi wa kifaa cha utafiti cha Airborne Gravity Gradiometer Survey bila ya kupata kibali cha bodi ya wakurugenzi ya shirika hilo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!