Wednesday , 27 September 2023
Home Habari Mchanganyiko Mkurugenzi Dodoma amaliza mgogoro wa ardhi wa miaka 20
Habari Mchanganyiko

Mkurugenzi Dodoma amaliza mgogoro wa ardhi wa miaka 20

Wakazi wa C Centre wakiwa katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji Dodoma. Picha ndogo Mkurugenzi wa Jiji, Godwin Kunambi
Spread the love

MKURUGENZI wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi amemaliza mgogoro wa ardhi uliodumu kwa zaidi ya miaka 20 kwa wakazi eneo la C Centre lililopo kata ya Nkuhungu Jiji la Dodoma. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma …. (endelea).

Kunambi amemaliza mgogoro huyo baada ya kikao cha pamoja kati makundi mawili ya wananchi waliokuwa na misimamo tofauti na timu ya maafisa ardhi wa Halmashauri ya Jiji kujadili namna ya kuwasaidia wananchi wa eneo hilo la C Centre katika ukumbi wa Jiji.

Mkurugenzi huyo amesema ipo haja ya serikali kuwasaidia wananchi hao kupata stahiki zao katika eneo hilo lakini wanatakiwa kuwa wakweli na waadilifu.

“Nataka kila mtu atambue kuwa yeye ni mvamizi kwenye eneo hili lakini serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli haiwezi kuwaacha wananchi wake wakataabika hivyo tumeamua kufanya hisani kwa kuhakikisha kila mtu apate kiwanja eneo hilo ili ajenge,” alisema Kunambi na kuongeza.

“Endapo mtu mwenye haki ya kupata eneo la C Centre akalikosa kwa sababu yoyote ile halmashauri itajitahidi kumtafutia eneo jingine lakini kwanza tumalize na hawa waliokuwa wakiishi hapo kwa miaka mingi na hawana mbadala wa mahali pengine pa kuishi.”

Kufuatia hatua hiyo makundi yaliyokuwa yakisigana kwa muda mrefu bila kupata suluhu na wengine kushindwa hata kusalimiana wameonyesha furaha yao mbele ya Mkurugenzi  wa Jiji na kuahidi kudumisha mshikamano katika eneo hilo.

Baadhi ya wajumbe waliowakilisha wananchi wanaishi katika eneo hilo wamemshukuru Mkurugenzi wa Jiji na kuahidi kusimamia utaratibu waliokubaliana kwa pamoja na kuhakikisha hakuna udanganyifu utakaojitokeza kwenye kuwatambua wananchi wanaotakiwa kupewa viwanja katika eneo hilo.

Kunambi ameahidi kupima upya eneo hilo ili kukidhi hitaji la wananchi hao na kuhakikisha zoezi hilo linakamilika ndani ya miezi miwili hadi kukamilika kwake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari Mchanganyiko

Wizara ya madini kurusha ndege ya utafiti wa madini Geita

Spread the loveKutokana na mchango wa wachimbaji wadogo wa madini kwenye pato...

Habari Mchanganyiko

Jafo aagiza kampuni za madini kuzingatia utunzaji mazingira, azitaka zijifunze kwa GGML

Spread the loveWAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia apewa tano ujenzi barabara Mtwara

Spread the loveWANANCHI wa Mkoa wa Mtwara, wameishukuru Serikali ya Rais Dk....

error: Content is protected !!