December 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge Chadema aitaka Serikali kutoa taarifa ya masoko

Frank Mwakajoka, Mbunge wa Tunduma

Spread the love

MBUNGE Tunduma, Frank Mwakajoka (Chadema) ameitaka serikali kutoa taarifa ya masoko kwa wafanyabiashara ya mahindi. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Mwakajoka alitoa kauli hiyo Bungeni alipokuwa akiuliza swali la nyongeza, amesema kuwa serikali imekuwa na tabia ya kuwazuia wafanyabiashara wa nafaka nje kwa kisingizio cha njaa. 

Aidha Mwakajoka ametaka kujua kama serikali ina mpango wa kuwatangazia masoko kwa kuwa bunge halionyeshwi moja kwa moja kutokana na hilo wafanyabiashara hawawezi kujua masoko yalipo.

Akijibu maswali hayo, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stella Manyanya amesema kuwa kwa sasa kuna chakula cha kutosha nchini hivyo ruksa kuuza chakula kwenye masoko ya nje.

Aidha Mhandisi Manyanya amesema kuwa wafanyabiashara wanaotafuta masoko wapitie wizara husika kwa kutumia simu au njia ya mitandao.

error: Content is protected !!