Monday , 5 June 2023
Home Habari Mchanganyiko Mkulima wa ndege kujipanga upya?
Habari MchanganyikoTangulizi

Mkulima wa ndege kujipanga upya?

Spread the love

NDEGE ya shirika la ndege la Tanzania (ATCL), iliyokuwa inashikiliwa kwa siku kadhaa katika uwanja wa ndege ya Oliver Tambo, hatimaye imerejeshwa nyumbani. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kurejeshwa nyumbani kwa kwa ndege hiyo, kunafuatia Mahakama nchini humo kutoa amri ya kufuta zuio lake la awali, lililoagiza ndege hiyo aina ya Airbus A220-300, kutoondoka nchini humo, hadi Mkulima wa kilowezi, Hermanus Steyn, atakapoliwa “fedha zake.”

Steyn anaidai serikali ya Tanzania, kiasi cha dola za Marekani 10 milioni (karibu Sh. 22 bilioni), kufuatia hatua ya serikali ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kutaifisha mashamba yake yaliokuwapo mkoani Arusha na baadaye kumuweka kizuizini.

Kuzuiwa kwa ndege hiyo, kulitokana na maombi yaliyowasilishwa mahakamani hapo na Hermanus Steyn, Mkulima wa Kilowezi aliyekuwa amepata kibali cha kuishikilia.

Dk. Damas Ndumbaro, naibu waziri wa mambo ya nje na uhusiano wa kimataifa nchini, ameiambia MwanaHALISI kuwa Jaji Twala M L amesema kuwa anamuru ndege hiyo kuachiwa.

Amesema, kama mkulima huyo bado ana madai yeyote, anapaswa kurudi kwenye mahakama za Tanzania na kusikilizwa.

Taarifa zinasema, Mkulima ambaye alipeleka shauri hilo mahakamani – Hermanus Steyn – na kupata kibali cha kushikiliwa ndege hiyo, hakuridhishwa na hukumu ya awali na kuamua kukata rufaa, ambako nako alishindwa.

“…serikali imeridhika na maamuzi ya Mahakama Kuu ya jimbo la Gauteng iliyoamuru ndege yetu iliyokuwa ikishikiliwa nchini Afrika Kusini kuachiwa mara moja,” ameeleza Dk. Ndumbaro katika mahojiano yake na mwandishi wa habari hizi.

Dk. Ndumbaro alikuwa mmoja wa mawakili waliowakilisha serikali katika shauri hilo.

Menejementi ya ATCL imetangaza kuwa itarejesha upya safari zake kati ya Dar es Salaam na Johannesburg, Ijumaa wiki hii.

Baada ya ya kushindwa kwa kesi ya awali na hatimaye rufaa, wakili wa Steyn amenukuliwa na BBC akisema, “…ni kushindwa moja kwa moja kwa haki, na mteja wangu anaona kuwa ameonewa. Bw. Steyn amepoteza kikomboleo cha mali na hii inamaanisha kuwa hawezi kukata rufaa bila ya ndege kuwa imezuiliwa.”

Jaji aliyesikiliza rufaa amesisitiza kuwa Afrika Kusini haina mamlaka ya kisheria (jurisdiction) ya kuliamulia jambo hilo.

Steyn alikuwa anamiliki ardhi, mifugo na mali nyingi ambazo zilitaifishwa na serikali miaka ya 1980.

Ilipofika miaka ya 1990 walikubaliana fidia atakayolipwa, kwa ujumla wake dola milioni 33 na tayari ameshalipwa dola milioni 20 kati ya hizo.

Hata hivyo, katika miaka ya hivi karibuni, serikali ya Tanzania, kwa mujibu wa mkulima huyo imeacha kulipa deni hilo, kitendo ambacho kilimsukuma kuiomba mahakama kuzuia ndege hiyo, ikiwa ni moja ya harakati zake za kutaka kumaliziwa deni lake.

Alipotakiwa maoni yake kuhusiana na kurejea kwa ndege hiyo, mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea alisema, amefurahishwa na hatua hiyo, lakini ametaka serikali kumalizana na mdaiwa wake.

“Kwa jinsi nilivyosikia, mahakama haikusema mkulima yule anayeidai serikali, hana haki. Hapana. Bali imesema, Mahakama za Afrika Kusini, hazina mamlaka ya kutekeleza maamuzi yaliyofanywa na mahakama za Tanzania,” ameeleza Kubenea.

Amesema, “kwa msingi huo, deni bado lipo na mkulima yule wa kilowezi, bado aweza kuendelea na madai yake katika mahakama nyingine nje ya Afrika Kusini.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Tunduma watenga 60 milioni kujenga machinjio ya kisasa

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma Imetenga kiasi cha Tshs Miloni 60...

Habari Mchanganyiko

Bilioni 17 kujenga bandari kavu Tunduma

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma iliyopo wilayani  Momba mkoani Songwe imepatiwa...

Habari Mchanganyiko

Bandari ya Kigoma kuongezewa uwezo wa kutoa huduma zake

Spread the love  SERIKALI kupitia mamlaka ya Bandari nchini (TPA), imewekeza takribani...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kifo cha mwanafunzi UDOM: Tume yamsafisha naibu waziri

Spread the loveTUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini (THBUB),...

error: Content is protected !!