April 12, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Airbus A220-300 iliyokamatwa Afrika Kusini yatua Tanzania

Spread the love

NDEGE ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), iliyokuwa imeshikiliwa nchini Afrika Kusini, tayari imetua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA). Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Ndege hiyo iliyokuwa imeshikiliwa kwa amri ya Mahakama Kuu ya Gauteng, Johannesburg imewasili JNIA tarehe 4 Septemba 2019 saa 2:25 usiku.

Kushikiliwa kwa ndege hiyo kulitokana na kesi ya fidia iliyofunguliwa mahakamani hapo na Hermanus Steyn dhidi ya Serikali ya Tanzania.

Katika kesi hiyo, raia huyo wa Afrika Kusini alieleza kuwa anaidai serikali ya Tanzania malipo yaliyobaki ya fidia ya mali zake zilizotaifishwa mwaka 1982.

Akipokea ndege hiyo JNIA, Profesa Palamagamba Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje alieleza furaha yake ambapo alisema, “Ni faraja kwa nchi kushinda kesi.”

Prof. Kabudi amewapongeza majaji wa Afrika Kusini kusimamia haki uliowezesha ndehe hiyo kuachwa huru na kurejea nchini. Hata hivyo ameeleza kutokuwa na wasiwasi wowote kwa ndege za Tanzania kukamatwa.

error: Content is protected !!