January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mkude mchezaji bora mwezi Desemba

Jonas Mkude

Spread the love

 

KIUNGO wa klabu ya Simba Jonas Mkude amechgauliwa kuwa mchezaji bora wa mashabiki wa klabu ya Simba mwezi Desemba kwenye tuzo za kila mwezi (Emirate Aluminium ACP Simba Fans Player of the Month). Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mkude ameshinda tuzo hiyo mara baada ya kuwabwaga walinzi wa kati wa kikosi hiko Josh Onyango sambamba na Henock Ingonga Baka ambao waliingia katika fainali ya kinyanga’anyiro hiko.

Katika mwezi Desemba, Mkude amecheza mechi nne kati ya tano akihusika katika upatikanaji wa mabao mawili (assist) huku akionyesha kiwango bora.

Mkude atakabidhiwa pesa taslimu Sh 2,000,000 pamoja na tuzo kutoka kwa Wadhamini Emirate Aluminium ACP kama sehemu ya zawadi.

Katika mchakato huo Mkude alipata kura 2397 sawa na asilimia 43.93, Onyango akipata kura 2393 sawa na asilimia 43.85 na Inonga akiambulia kura 667 sawa na asilimia 12.22.

error: Content is protected !!