Saturday , 22 June 2024
Habari za Siasa

Mkapa sasa aonywa

Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu
Spread the love

VIONGOZI wandamizi serikalini wameonywa kutojihusisha na matamshi ya kejeli na matusi dhidi ya wananchi, kwa kuwa yanachochea chuki na uhasama nchini, anaandika Mwandishi wetu.

Onyo hilo limetolewa jijini Dar es Salaam na wiki hii na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bahame Tom Nyanduga, kufuatia matamshi ya rais mstaafu Benjamin Mkapa aliyewatuhumu wananchi wanaoikosoa serikali iliyopo madarakani.

Amesema, matamshi yanayolenga kuwakejeli wananchi yanaweza kuhatarisha usalama wa nchi kwa kuwa yanapandikiza chuki na kuchochea uhasama.

Akizungumza mjini Chato, mkoani Geita, Jumanne iliyopita, Mkapa aliwaita wananchi wenye mtazamo tofauti na ule wa serikali juu ya huduma za afya, kuwa ni  “wapumbavu na “malofa.”

“Tume inasema, kauli ya Mkapa ni kejeli kwa wananchi. Haiheshimu mawazo ya watu wengine wenye mtazamo tofauti kuhusiana na suala zima la maendeleo ya afya katika jamii,” ameeleza Nyanduga.

Amesisitiza, “Tume inaamini kuwa matamshi haya ya Mkapa ni kinyume cha haki ya kila mtu kuwa na maoni tofauti. Kauli hiyo pia inapingana na na kauli za viongozi kuwa kampeni za uchaguzi ziliisha na sasa tufanye maendeleo.”

Hii ni mara ya pili kwa kiongozi huyo wa awamu ya tatu kutoa kauli za kebehi na matusi dhidi ya  wananchi.

Akihutubia mkutano wa kampeni wa chama chake – Chama Cha Mapinduzi (CCM) – katika uchaguzi mkuu wa  mwaka 2015, Mkapa aliwaita wananchi wanakikosoa chama chake kuwa “wapumbavu na malofa.”

Mkapa alikuwa rais wa Jamhuri ya Muungano kati ya mwaka 1995 na 2005.

Katika kipindi chake cha miaka 10 ya urais, utawala wake ulikumbwa na kashifa lukuki, ikiwamo uuzaji; na au ugawaji holela wa nyumba za serikali, migodi na mashamba; ubinafsishaji wa mashirika nyeti ya umma, ikiwamo iliyokuwa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), kampuni ya simu (TTCL) na shirika la ndege la taifa (ATC).

Aidha, utawala wa Mkapa ulibariki au kunyamazia mauaji ya makumi ya raia, katika machafuko ya kisiasa ya 26 na 27 Januari 2011, Visiwani Unguja.

Anataja anachoita, “vimeo vya Mkapa” kuwa ufisadi katika ugawaji wa mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira, nyumba za serikali, uuzaji wa NBC (Benki ya Taifa ya Biashara) na ukwapuaji wa mabilioni ya shilingi katika akaunti ya madeni ya nje (EPA), ndani ya Benki Kuu (BoT).

Kabla na baada ya kuondoka madarakani, Mkapa amekuwa akitajwa na kuhusishwa na baadhi ya tuhuma za ufisadi na utovu wa “utawala bora” wakati wa kipindi chote cha utawala wake – 1995 hadi 2005.

Ametuhumiwa kujimilikisha mgodi wa mkaa wa mawe wa Kiwira mkoani Mbeya kupitia kampuni yake ya ANBEN anayomiliki na mkewe, Anna Mkapa ikiwa miongoni mwa makampuni matano yaliyoingia ubia na kampuni ya TanPower Resources Company Limited.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yaahidi kushirikiana na Prof. Ndakidemi kuhamasisha zao la kahawa

Spread the loveSerikali imeahidi kuungana na Mbunge wa Moshi Vijijini, Profesa Patrick...

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

IMF yaimwagia Tanzania trilioni 2.4 kukabili mabadiliko ya hali ya hewa

Spread the loveShirika la Kimataifa la Fedha (IMF) jana Alhamisi limesema bodi...

Habari za SiasaKimataifa

Mmoja afariki, 30 wajeruhiwa maandamano Kenya

Spread the loveMtu mmoja ameripotiwa kuuawa na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape awaomba wadau wa habari wamuamini

Spread the loveWAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

error: Content is protected !!