Wednesday , 6 December 2023
Home Kitengo Biashara Milioni 40 kujenga stendi ndogo Tunduma
Biashara

Milioni 40 kujenga stendi ndogo Tunduma

Spread the love

HALMASHAURI ya mji Tunduma wilayani Momba mkoani Songwe imetenga Sh 40 milioni kujenga stendi ya magari madogo zikiwemo daladala aina ya Hiace kwa fedha zake za mapato ya ndani ili kupunguza adha za usafirishaji mkoani Songwe. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe…(endelea).

Hayo yameelezwa jana Jumatatu na Mkurugenzi mtendaji wa mji Tunduma, Philimon Magesa katika kikao cha baraza la madiwani.

Amesema kutokana na uwepo wa stendi kuu Mpemba wameamua kujenga stendi ndogo iuli kupunguza msongamano kwenye stendi hiyo.

Amesema baada ya serikali kuwapatia fedha kujenga stedi kuu iliyopo kata ya Mpemba na halmashauri kutoa Sh 500 milioni za mapato ya ndani kujenga barabara ya kiwango cha lami eneo la kuzunguka soko, pia wametoa tena Sh 40 milioni kujenga stendi ya kugeuzia gari ndogo eneo la Chipaka.

“Stendi hiyo ni kwa ajili ya gari ndogo zikiwemo Hiace zinazotoka Mlowo hadi stendi ya Mpemba ili zikishusha abiria ziende hadi stendi ya Chipaka kushusha mizigo na kupakia abiria kisha kurudi stendi ya mpemba” amesema Magesa.

Naye Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Ayoub Mlimba amesema lengo la kujenga stendi hiyo ni kupunguza adha zilizopo kwani Tunduma ni mji wa kibiashara.

Amesema  stendi hiyo itarahisisha abiria wakiwemo wafanyabiashara kupeleka bidhaa zao maeneo ya masoko yaliyopo Mjini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

CEO NMB ashiriki mkutano wa Benki ya Dunia

Spread the loveAfisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna ameshiriki...

Biashara

Jisajili Meridianbet kasino msimu huu wa Sikukuu upate mgawo wa Mil 2.5

Spread the love  UNAIJUA 200% inakuaje? Meridianbet msimu huu wa Sikukuu za...

BiasharaTangulizi

Bei ya Dizeli, Petroli yashuka

Spread the loveBEI ya mafuta kwa mwezi Disemba, imeshuka kutokana na kupungua...

Biashara

GGML yataja mbinu kuimarisha miradi ya ujenzi, Bashungwa atoa maagizo

Spread the loveKATIKA kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan kuimarisha...

error: Content is protected !!