Friday , 17 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wananchi Songwe watakiwa kuachana imani potofu kudhiti ukatili
Habari Mchanganyiko

Wananchi Songwe watakiwa kuachana imani potofu kudhiti ukatili

Spread the love

WANANCHI wa wilaya zilizopo mkoa wa Songwe wametakiwa kuishi kwa kufanya kazi kihalali na kumtegemea Mungu na kuacha kujiingiza kwenye imani za kishirikina kwa lengo la kujipatia utajiri kwa kudhuru watu. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe …(endelea).

Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Katibu tawala mkoa wa Songwe, Happiness Seneda  wakati akizungumza na wakazi wa Msia na Iziyeniche katika hitimisho la ziara yake ya kukagua miradi na kuzungumza na wananchi ambao aliwataka watoe kero zinaźowakabiri.

Alisema Songwe ni moja ya mikoa yenye unyanyasaji wa watoto ikiwamo ubakaji vitendo vinavyotokana na imani za kishirikina kwa lengo la kupata utajiri.

“Acheni imani hizo, viongozi ngazi ya vijiji, kata, wilaya hadi mkoa… toeni elimu ili jamii iache vitendo hivyo,” alisema.

Ndivane Zewanga mkazi wa kijiji cha Iziyeniche alidai kuwa kumekuwapo na unyanyasaji kwa baadhi ya wazazi wakiwatuma watoto chini ya miaka saba kununua sigara na pombe vilabuni badala ya kuwahamasisha kwenda shule.

Zewanga aliungwa mkono na Imanuel Mtafya mkazi wa kijiji hicho ambaye alisema kuna matukio mengi yanayofanyika ikiwemo ya ubakaji na ukatili lakini wahanga huogopa kusema wakihofia kunyooshewa vidole hali ambayo inahitaji elimu ili kukomesha matendo hayo.

Akizungumzia matukio hayo, Katibu tawala mkoani humo, Happiness Seneda  aliwataka wananchi kuwatunza watoto, na kuachana na vitendo vya kikatili ikiwemo ubakaji, akisema baadhi wamekuwa na imani potofu kuwa kwa kujihusisha na ubakaji mtoto ili kupata utajiri.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari Mchanganyiko

Wananchi washauriwa kuongeza uelewa wa kujikinga na majanga

Spread the love WITO umetolewa kwa wananchi kuongeza uelewa na utayari kabla...

error: Content is protected !!