Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mikoa sita yenye udumavu Tanzania yatajwa
Habari Mchanganyiko

Mikoa sita yenye udumavu Tanzania yatajwa

Spread the love

SERIKALI ya Tanzania imetaja mikoa sita inayoongoza kwa tatizo la udumavu, kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mikoa hiyo inaongozwa na Njombe yenye asilimia 53.6 ya watoto wenye tatizo hilo, ikifuatiwa na Rukwa (47.9%), Iringa (47.1%), Songwe (43.3%), Kigoma (42.3%) na Ruvuma (41.0%)

Hayo yamesemwa leo Jumanne tarehe 19 Mei, 2020 na wizara ya kilimo wakati ikijibu swali la Dunstan Kitandula, Mbunge wa Mkinga (CCM), aliyehoji mkakati wa serikali katika kukabiliana na tatizo la utapiamlo nchini.

Katika swali lake ambalo limejibiwa kwa njia ya mtandao, Kitandula amesema utapiamlo ni janga kubwa nchini kwa kuwa kati ya watoto 100, watoto 30 wana tatizo la udumavu wa akili, huku kati ya watoto 100, watoto 59 wana tatizo la upungufu wa damu.

Kitandula amesema changamoto hiyo inasababisha Serikali kutumia fedha nyingi kukabiliana na tatizo hilo, ambazo zingeweza kutumika katika sehemu nyingine, kama kilimo kingeboreshwa ili kuwezesha upatikanaji wa mazao ya lishe bora.

Akijibu swali hilo, waziri wa kilimo amesema, wizara yake imeanza kutoa mafunzo ya uzalishaji, utayarishaji na ulaji wa vyakula vilivyoongezwa virutubishi katika mikoa yenye asilimia kubwa ya tatizo la udumavu kwa watoto.

“Mafunzo haya yanalenga kujengea uwezo wa jamii, katika kuzalisha na kutumia mazao yaliyoongezewa virutubishi kibaiyolojia, hatimaye kukabiliana na upungufu wa vitamini na madini mwilini hususan watoto,  chini ya miaka mitano na kina mama wajawazito na wanaonyonyesha,” amejibu.

Amesema wizara ya kilimo inashirikiana na wizara nane zinazohusika na masuala ya lishe nchini, kutekeleza mpango jumuishi wa kitaifa wa lishe, ili kutokomeza tatizo hilo.

“Aidha kwa kushirikiana na wizara ya viwanda na biashara, virutubishi vinaongezwa (Fortification) katika baadhi ya bidhaa zenye matumizi makubwa. Kwa mfano, madini chuma, Zinki na Vitamini B9 (Folic acid) huongezwa kwenye unga, ambapo Vitamini A huongezwa katika mafuta ya kupikia,” amesema Hasunga na kuongeza:

“Wizara pia, ina jukumu la kuelimisha jamii kuhusu uzalishaji wa mazao mchanganyiko (crop diversification) na matumizi ya vyakula vinavyotokana na mazao hayo.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!