Saturday , 9 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mgombea wa 17 achukua fomu ya urais Tanzania
Habari za Siasa

Mgombea wa 17 achukua fomu ya urais Tanzania

Spread the love

MGOMBEA urais wa Tanzania kupitia Chama Cha NLD, Maisha Mapya Muchunguzi amekabidhiwa fomu za uteuzi wa urais na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Semistoles Kaijage. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Muchunguzi amekabidhiwa fomu hizo leo Jumatano tarehe 19 Agosti 2020 katika ofisi ndogo za NEC zilizopo jijini Dar es Salaam.

Muchunguzi amekuwa mgombea wa 17 kujitosa kwenye mbio hizo za kuwania kuteuliwa na NEC kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020.

Vyama vyenye usajili wa kudumu nchini Tanzania ni 19, vyama viwili vya UDP na TLP havijajitosa kwenye kinyang’anyiro hicho kwa sababu vimekwisha weka wazi kumuunga mkono mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais John Pombe Magufuli.

Idadi hiyo ya wagombea 17 ni kubwa ukilinganisha na uchaguzi uliopita mwaka 2015 ambapo waliochukua fomu walikuwa 11, walioteuliwa na NEC kugombea walikuwa nane, wawili hawakurejesha fomu na mmoja alirejesha nje ya muda uliokuwa umepangwa.

Kati ya hao 11, mwanamke alikuwa mmoja ambaye ni Anna Mgwhira aliyegombea kupitia chama cha ACT- Wazalendo.

Anna ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, tarehe 3 Juni 2017, Rais Magufuli alimteua kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro nafasi anayohudumu mpaka sasa.

Mwaka huu, kati ya wagombea 17 waliochukua fomu, wanawake ni wawili ambao ni Cecilia Augustino Mwanga wa chama cha Demokrasia Makini na Qeen Cuthbert Sendiga wa chama cha ADC huku wagombea wenza kati ya 17 ni watano.

Shughuli ya uchukuaji na urejeshaji wa fomu ulianza tarehe 5 Agosti na utahitimishwa 25 Agosti 2020 siku ambayo Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) itafanya uteuzi wa wagombea.

Kampeni za uchaguzi huo zitaanza tarehe 26 Agosti hadi 27 Oktoba 2020 ikiwa ni siku 62.

Wagombea wengine waliochukua fomu ni; Yeremia Maganja (NCCR-Mageuzi), Seif Maalim Seif (AAFP), Leopard Mahona (NRA), Profesa Ibrahim Lipumba (CUF), Philip John Fumbo (DP) na David Mwaijojele wa Chama Cha Kijamii (CCK).

Wengine ni; Khalfan Mohamed Mazurui (UMD), Twalib Ibrahim Kadege (UPDP), Rais John Pombe Magufuli (CCM), Bernard Membe (ACT- Wazalendo), Tundu Lissu (Chadema), Mutamwega Bati Mgaiwa (SAU), Hashim Rungwe (Chaumma) na John Shibuda wa Ada Tadea.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mbowe: Miaka 62 ya uhuru tujenge upya mioyo yetu

Spread the loveWAKATI Tanganyika ikiadhimisha miaka 62 tangu kupata uhuru, Mwenyekiti wa...

Habari za Siasa

Rais Samia asamehe wafungwa 2,244

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewasamehe wafungwa 2,244, huku akiwabadilishia...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataka jamii inayohoji mafisadi

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan ametoa maagizo juu ya uboreshaji dira...

Habari za SiasaTangulizi

Kapinga: Kukatika kwa umeme siyo hujuma

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema Serikali ipo kazini...

error: Content is protected !!