Sunday , 28 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Meneja TARURA Kilombero atumbuliwa
Habari Mchanganyiko

Meneja TARURA Kilombero atumbuliwa

Spread the love

 

MTENDAJI Mkuu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Mhandisi Victor H. Seff amemuondoa kwenye majukumu yake aliyekuwa Meneja wa TARURA Wilaya ya Kilombero kwa kushindwa kusimamia kikamilifu miradi.

Miradi ambayo meneja huyo ameshindwa kusimamia ni pamoja ujenzi wa Boksi Kalavati katika Barabara ya Mawala-Mofu-Ikwambi kilomita 30 iliyopo Halmashauri ya Mlimba, Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro. Anaripoti Mwandishi Wetu, Morogoro … (endelea).

Hayo yamejiri baada ya Kiongozi huyo kufanya ziara ya ukaguzi wa miradi wilayani Kilombero na kubaini kasoro katika usimamizi wa miradi ikiwemo ujenzi wa boksi kalavati katika barabara hiyo ambayo imejengwa chini ya viwango vya mkataba hali iliyompelekea kumuondoa mara moja Meneja wa TARURA wa wilaya hiyo.

“Nimekagua na kujiridhisha kwamba mradi huu umejengwa chini ya kiwango, kwa kweli sijaridhishwa na usimamizi wa hapa, hivyo nimemuondoa kwenye nafasi yake kuanzia leo aliyekuwa Meneja wa TARURA Wilaya ya Kilombero na atapangiwa majukumu mengine,” alisema Mhandisi Seff.

Aidha, Mtendaji Mkuu amemtaka Mkandarasi aliyejenga mradi huo chini ya viwango vya mkataba kubomoa kwa gharama zake na kukamilisha ujenzi wa Boksi Kalavati jipya ndani ya kipindi cha mwezi mmoja.

Pia, Mhandisi Seff amewataka Mameneja wa TARURA nchi nzima kusimamia kikamilifu miradi kwenye maeneno yao na kwamba hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atayeshindwa kutimiza majukumu yake ili kuhakikisha fedha inayotolewa na Serikali inaendana na ubora wa miradi inayotekelezwa.

Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) unaendelea na kazi ya kusimamia ujenzi, ukarabati na matengenezo ya mtandao wa barabara za Wilaya wenye jumla ya KM 144,429.77 nchi nzima ili kuhakikisha wananchi wanazifikia huduma za kijamii na kuendeleza shughuli zao za kiuchumi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wami Ruvu hawana deni la Rais Samia katika kutunza vyanzo vya maji

Spread the love  BODI ya Maji Bonde la Wami Ruvu, imeendelea kuchua...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari Mchanganyiko

Dk. Jafo aipongeza Oryx kumuunga mkono Samia

Spread the loveWAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na...

Habari Mchanganyiko

Mvungi aendesha kikao kazi cha wataalam wa Regrow

Spread the love  MKURUGENZI wa Idara Sera na Mipango Wizara ya Maliasili...

error: Content is protected !!