Thursday , 28 March 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Ufaransa kuwapiga msasa wanajeshi 2000 wa Ukraine
Kimataifa

Ufaransa kuwapiga msasa wanajeshi 2000 wa Ukraine

Spread the love

 

WAKATI vita kati ya Urusi na Ukraine ikiendelea kupamba moto, Taifa la Ufaransa limetangaza kuanza kuwapa mafunzo maalumu wanajeshi 2,000 wa Ukraine kwa wiki kadhaa. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Hayo yameelezwa na Waziri wa Ulinzi, Sébastien Lecornu kwenye Gazeti la Le Parisien toleo la jana tarehe 16 Oktoba, 2022.

Hii ni mara ya kwanza kwa Ufaransa kujitolea kuratibu wa mafunzo ya kijeshi ya aina yake tangu kuanza kwa mgogoro wa kijeshi nchini Ukraine.

Ufaransa ilikuwa tayari imewapokea wapiganaji wa Ukraine ili kuwafundisha jinsi ya kutumia bunduki maarufu za Caesar, lakini wakati huu programu iliyotangazwa na Sébastien Lecornu ni ukubwa na ya tofauti.

Wanajeshi 2,000 watapokelewa nchini Ufaransa kwa mafunzo katika ngazi tatu: mafunzo ya jumla ya wapiganaji, vifaa na mafunzo kuhusu vifaa vinavyotolewa na Ufaransa.

Tangu kuanza kwa mzozo huo, nchi zingine mbali na Ufaransa zimepokea wanajeshi wa Ukraine kwa mafunzo katika nchi zao, hasa Uingereza.

Mafunzo ya vifaa yatahusu bunduki za Caesar, lakini pia makombora ya kulipua vifaru yaitwayo Milan, makombora ya kudungua ndege yaitwayo Mistral na hivi karibuni mfumo wa ulinzi wa makombora uitwao Crotale.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanaye rais jela miaka miaka 6 kwa dawa za kulevya

Spread the loveMwanawe rais wa zamani wa Guinea-Bissau amehukumiwa kifungo cha miaka...

Habari za SiasaKimataifa

Faye aahidi kuongoza kwa unyenyekevu, wagombea wenzie wakubali yaishe

Spread the loveMgombea wa upinzani Senegal, Bassirou Diomaye Faye anajiandaa kuwa rais...

Habari MchanganyikoKimataifa

Wanafunzi 130 waliokuwa wametekwa nyara waokolewa

Spread the loveZaidi ya wanafunzi 130 wa shule ya msingi LEA na...

Habari MchanganyikoKimataifa

Mgombea upinzani aongoza uchaguzi wa Rais Senegal

Spread the loveMgombea wa upinzani nchini Senegal, Bassirou Diomaye Faye ameonekana kuongoza...

error: Content is protected !!