April 12, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Meneja reli ya SGR abambwa akitorosha fedha

Dola za Marekani

Spread the love

YETKIN Gen Mehmen, Meneja Uwezeshaji wa Kampuni ya Yapi Merkezi, inayojenga mradi wa reli ya kisasa (SGR) nchini Tanzania, amehukumiwa kwenda jela miaka mitatu ama kulipa faini ya Sh. 100 milioni pia kutaifishwa Dola za Marekani 84,850 alizokutwa nazo. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Leo tarehe 27 Februari 2020, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam imetoa hukumu hiyo baada ya kuthibitika, kwamba Yetkin alitaka kusafirisha fedha hizo nje ya nchi kinyume cha sheria.

Bosi huyo wa SGR ambaye ni raia wa Uturuki, alikutwa na ‘mzigo’ huo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), tarehe 13 Februari 2020.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hivyo, Yetkin amekiri kushindwa kufuata taratibu ikiwa ni pamoja na kushindwa kutoa maelezo kuhusu kitita cha fedha alichokutwa nacho JNIA.

Hakimu Simba amesema, kwa kuwa Yetkin amekiri kosa hilo, amehukumiwa kulipa faini ya Sh. 100 milion ama kwenda jela miaka mitatu ikiwa ni pamoja na kutaifishwa fedha hizo na kuwa mali ya Serikali ya Tanzania.

Shadrack Kimaro, Wakili wa Serikali Mkuu alimsomea mtuhumiwa huo mashtaka kwamba tarehe tajwa alikamatwa NJIA akiwa na begi la mkononi lenye kiasi hicho cha fedha na kwamba, alishindwa kutoa ufafanuzi kuhusu fedha hizo.

error: Content is protected !!