Monday , 4 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Membe afukuzwa CCM, Kinana chini ya uangalizi
Habari za SiasaTangulizi

Membe afukuzwa CCM, Kinana chini ya uangalizi

Spread the love

BERNARD Membe, Waziri wa Mambo ya Nje mstaafu amefukuzwa uanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM), huku Abdulrahman Kinana, aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, akiwekwa chini ya uangalizi kwa muda miezi 18. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Adhabu hizo zimetolewa leo tarehe 28 Februari 2020 na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM baada ya kupitia taarifa ya mahojiano kuhusu tuhuma zilizokuwa zinawakabili makada hao, katika kikao chake kilichofanyika jijini Dar es Salaam, chini ya Dk. John Magufuli, mwenyekiti wa chama hicho.

Akitangaza maamuzi ya kamati hiyo, Humphrey Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, amesema Membe amefukuzwa uanachama kutokana na kushindwa kubadili muenendo wake ndani ya chama hicho tangu mwaka 2014, licha ya kupewa adhabu mara kadhaa.

“Kamati imeazimia kwa kauli moja kwamba Membe afukuzwe uanachama wa CCM, uamuzi huu umekuja baada ya kuwa taarifa zake ndani ya chama zinaonesha mwenendo wake kutoka mwaka 2014 kubadilika,” amesema Polepole na kuongeza:

“Ambako katika chama amewahi kupata adhabu nyingine ambazo zingeweza kumsaidia kujirekebisha lakini imeonekana sivyo, kwa hiyo narudia tena adhabu yake kamati imeazimia kwa kauli moja afukuzwe uanachama.”

Kuhusu Kinana, Polepole amesema kamati hiyo imempa adhabu ya karipio kali, ambapo kwa mujibu wa katiba ya CCM mwanachama atakayekutwa na adhabu hiyo, atakuwa chini ya uangalizi kwa muda wa miezi 18.

“Kamati kuu imepokea maelezo na imeazimia ndugu Kinana apewe adhabu ya karipio kwa mujibu  wa kanuni za uongozi na maaidli, adhabu imeanishwa katika kanuni na inasema, mwanachama anayefanya kosa linalokipaka tope chama bila kuonesha nia ya kujirekebisha, kamati inaweza kumpa mwanachama huyo adhabu ya karipio.

Atakuwa kwenye hali ya matazamio muda miezi isiyopungua miezi 18 kutoka tarehe ya leo 28 Februari 2020, ili kumsaidia mwanachama huyu katika jitihada za kujirekebisha akiwa kwenye kipindi hicho hatakuwa na haki ya kugombea nafasi yoyote katika chama lakini atakuwa na haki ya kupigia kura,” ameeleza Polepole.

Wakati huo huo, Polepole amesema kamati hiyo imemsamehe Mzee Yusuph Makamba, Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM, kutokana na kada huyo kuwa muungwana kwa kuandika barua ya kuomba msamaha.

“Kamati kuu ya halmshauri kuu ya taifa, imeazimia kwa kauli moja kwamba, kutoa msamaha kwa  Mzee Makamba  kwa msingi kwamba wakati wote tangu aliposomewa mashtaka yake amekuwa mtu muungwana, ameomba asamehewe makosa yake kwa barua,” amesema Polepole.

Makada hao watatu walihojiwa na Kamati Ndogo ya Nidhamu na Udhibiti ya CCM, kufuatia tuhuma zilizokuwa zinawakabili za kukiuka maadili ya chama hicho.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Mwinyi aungana na Samia kuuaga mwili wa baba yake

Spread the loveRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk....

Habari za SiasaTangulizi

Mtoto wa Mzee Mwinyi amwaga machozi

Spread the loveMtoto wa Hayati mzee Mwinyi, Abdullah Ali Hassan Mwinyi ameshindwa...

Habari za SiasaTangulizi

Mzee mwinyi alikuwa mwanademokrasia wa kweli

Spread the loveMtoto wa Hayati Ali Hassan Mwinyi, Abdullah Ali Hassan Mwinyi...

Habari za SiasaTangulizi

Samia: Mwinyi alikuwa maktaba inayotembea

Spread the loveRais Samia Suluhu hassan amesema Hayati rais mstaafu, Ali Hassan...

error: Content is protected !!