October 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rugemalira kuruka kihunzi hiki?

James Rugemalira, mfanyabiashara na Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP

Spread the love

JAMES Rugemalira, mfanyabiashara na Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP na mmiliki wa zamani wa Kampuni ya IPTL, anapambana kujinasua katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Leo tarehe 27 Februari 2020, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam imekubali ombi lale ka kuwasilisha hoja za kutaka aachiwe huru.

Rugemalira na Mkurugenzi wenza wa IPTL, Habinder Sethi na mwanasheria wa kampuni hiyo Joseph Makandege wanakabiliwa na kosa la uhujumu uchumi mahakamani hapo.

Katika harakati zake, Rugemarila amewasilisha ombi hilo leo wakati shauri hilo lilipotajwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Rugemarila kupitia wakili wake John Chuma, amedai kuwa mteja wake ameshawasilisha hoja za pingamizi la awali lakini hajapata majibu yoyote kutoka upande wa Jamuhuri.

Akijibu hoja hizo, wakili wa serikali Wankyo Simon amedai, baadhi ya nyaraka amezipata leo mahakamani hapo, na kuwa upande wa Jamuhuri upo tayari kusikiliza hoja hizo kwa njia ya mdomo kama nyaraka hizo zimeingizwa kwenye kumbukumbu ya mahakama, hata kwa wakati huo kama ratiba ingeruhusu.

Wankyo pia amedai, mshtakiwa wa pili amekua anajiwasilisha mwenyewe huku akiwa na uwakilishi wa mawakili, hivyo anapaswa kusema kama amewaacha au wanaendelea

Akijibu suala hilo, Rugemarila amedai kuwa amekua na wawakilishi hata zaidi ya 30, lakini kuna hoja lazima aziwasilishe mwenyewe na kuwa hilo jambo walitakiwa kulalamika mawakili wake na sio yeye, kwani sheria inamruhusu kujiwakilisha.

Baada ya hoja hizo, Hakimu Shaidi ameahirisha shauri hilo hadi tarehe 12 Mach 2020, shauri hilo litakuja kutajwa na upande wa Jamuhuri utawasilisha majibu.

Washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza tarehe 196 Juni 2017. Washitakiwa hao wanadaiwa, tarehe 18 Oktoba 2011 na tarehe 19 Machi 2014 jijini Dar es Salaam, walikula njama katika nchi za Afrika Kusini, Kenya na India ili kutenda kosa.

Aidha, inadaiwa katika mashitaka ya kujipatia fedha kwamba, kati ya tarehe 28 Novemba na 29 mwaka 2011 na tarehe 23 Januari 2014, Makao Makuu ya Benki ya Stanbic, Kinondoni na Benki ya Mkombozi Tawi la Mtakatifu Joseph, kwa ulaghai washitakiwa hao walijipatia kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Dola za Marekani 22,198,544.60 na Sh 309, 461,300,158.27.

Pia washitakiwa wote wanadaiwa kuisababishia serikali hasara, ambapo inadaiwa walitenda makosa hayo tarehe 29 Novemba 2013 katika Benki ya Stanbic, Tawi la Kati Kinondoni, kwa vitendo vyao waliisababishia serikali hasara ya Dola za Marekani 22, 198, 544.60 na Sh 309,461,300,158.27.

Kati ya tarehe 29 Novemba 2013 na tarehe 23 Januari 2014 maeneo tofauti Dar es Salaam, kwa pamoja walitenda kosa la kutakatisha fedha kwa kuchukua fedha kutoka BoT, ambazo ni Dola za Marekani milioni 22.1 na Sh bilioni 309.4 wakati wakijua fedha hizo ni zao la kujihusisha na genge la uhalifu.

error: Content is protected !!