August 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Meena awaomba radhi wanahabari

Paul Makonda, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam (katikati) akizungumza na Theophil Makunga, Mwennyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania na Naville Meena, Katibu wa Jukwaa hilo

Spread the love

NEVILE Meena, Katibu Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), amewaomba radhi waandishi wa habari na Wahariri, anaandika Hellen Sisya.

Msamaha huo unafuatia Meena kutoa kauli kwamba kuanzia leo, wamemfungulia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambaye wanahabari walisusa kuandika habari zake.

Kauli hiyo ya kutaka Makonda afunguliwe iliyoonyesha kuwachukiza waandishi wa habari.
Katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, Meena ameandika ujumbe maalum wa kuomba radhi wanahabari.

Ametumia maneno ya kiingereza “We have messed up. My apologies to all journalists and media professionals” ameandika Meena.

Mapema leo hii Jukwaa hilo la wahariri liliitisha mkutano na wanahabari na kumfungulia kifungo RC Makonda, kifungo ambacho walimfungia kuandika na kuripoti taarifa zake.

Makonda alifungiwa baada ya kuvamia kituo cha TV cha Clouds cha jijini Dar es Salaam na kutaka kulazimisha habari ya uongo kutangazwa dhidi ya  Mchungaji, Josephat Gwajima.

error: Content is protected !!