Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko MCT: Rais Samia ameibua matumaini
Habari Mchanganyiko

MCT: Rais Samia ameibua matumaini

Spread the love

 

BARAZA la Habari Tanzania (MCT), limepongeza hatua ya Rais Samia Suluhu Hassan, kukataza ubabe katika kufungia vyombo vya habari. Anaripoti Yusuph Katimba, Dar es Salaam…(endelea).

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Kajubi Mukajanga, Katibu Mtendaji (MCT) amesema, Rais Samia ameonesha umuhimu wa kudurusu sheria na kanuni zinazohusu tasnia ya habari.

Kajubi ameeleza, hotuba Rais Samia aliyoitoa Jumanne ya tarehe 6 Aprili 2021 kwa taifa wakati akiwaapisha Makatibu Wakuu, Manaibu Makatibu Wakuu na wakuu wa taasisi mbalimbali za umma, imeibua matumaini.

“Hotuba hiyo imetoa mwanga pia wa uwezekano wa kuzidurusu sheria za habari na kanuni zake, na hivyo kuzifanyia marekebisho yanayotakiwa ili nchi yetu iwe ya taifa linaloongea na kujadiliana kwa uhuru.

“Wadau wa habari wamepokea agizo la kwenye hotuba ya Mhe. Rais Samia S. Hassan, la kuwataka viongozi kuwa makini na kuacha kutumia ubabe kufungia vyombo vya habari kwa furaha na matumaini makubwa,” ameeleza.

Kwenye taarifa hiyo Kajubi amesema, kwa kipindi kirefu sekta ya habari imekuwa ikipitia kipindi kigumu katika kutekeleza majukumu yake ya kuhabarisha umma, kipindi ambacho kimeshuhudia vyombo vingi vya habari vikifungiwa kwa muda na vingine kupotea kabisa.

Amesema, pamoja na hotuba nzuri ya Rais Samia, MCT linawakumbusha waandishi wa habari kuwa, ngao kubwa ya kuwalinda kama wanataaluma ni kufuata maadili ya uandishi wa habari ambayo tasnia imejiwekea yenyewe.

“Uhuru unakuja na uwajibikaji, hivyo wanahabari wazingatie weledi na maadili ya uandishi.

“Kufuatia agizo la Mhe. Samia, baraza linaamini viongozi wenye jukumu la kusimamia vyombo vya habari watatekeleza maagizo ya Rais mara moja, bila visingizio au mikwara kama tulivyoona pale vyombo vya habari viliposhinda kesi mahakamani, bado havikufunguliwa,” ameeleza.

Hata hivyo amesema, sheria na kanuni mbovu zitafanya nia nzuri ya Rais Samia ififie katika utendaji, kwani vyombo vilivyofungiwa vinaweza kufunguliwa leo lakini vikafungwa tena muda mfupi baadaye kwa kutumia mianya iliyoko katika sheria.

“Baraza linaikumbusha serikali kuwa, kuna hukumu ya Mahakama ya Afrika Mashariki iliyotolewa Machi 28, 2019 iliyoagiza vipengele 16 vya Sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari virekebishwe, ambayo haijafanyiwa kazi.

“Wadau tunaiomba serikali kuifanyia kazi na tuko tayari kutoa ushirikiano wote, kwani sote tunajemga nyumba moja,” ameeleza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!