January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Mwigulu ataja sababu ongezeko deni la Taifa

Dk. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango

Spread the love

 

WAZIRI wa Fedha na Mipango nchini Tanzania, Dk. Mwigulu Nchemba, ametoa sababu ya kuongezeka kwa deni la taifa, kutoka Sh.54.8 trilioni mwaka 2019 hadi Sh.59 trilioni mwaka 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Amesema, ongezeko hilo ni sawa na asilimia 7.6.

Dk. Mwigulu amesema hayo leo Alhamisi, tarehe 8 Aprili 2021, bungeni jijini Dodoma, wakati akiwasilisha mapendekezo ya serikali ya mpango wa maendeleo ya taifa na kiwango cha ukomo wa bajeti ya serikali kwa mwaka 2021/22.

Waziri huyo amesema, kati ya kiasi hicho, deni la nje ni Sh.42.8 trilioni 42.8 na deni la ndani Sh.16.2 trilioni.

Akielezea sababu zilizochagiza kuendezeka, Dk. Mwigulu amesema “kupokelewa kwa fedha za mikopo kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara, reli, viwanja vya ndege, umeme na maji.”

“Na malimbikizo ya riba ya deni la nje, hususan nchi zisizo wanachama wa kundi la Paris Club ambazo Serikali inaendelea kujadiliana nazo.”

“Aidha, matokeo ya tathmini ya uhimilivu wa deni iliyofanyika Desemba 2020 yanaonesha kuwa deni ni himilivu kwa muda mfupi, wa kati na mrefu,” amesema

error: Content is protected !!