Tuesday , 19 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu, Prof. Safari: Dk. Hoseah chaguo sahihi TLS
Habari za SiasaTangulizi

Lissu, Prof. Safari: Dk. Hoseah chaguo sahihi TLS

Dk. Edward Hoseah
Spread the love

 

GWIJI wa sheria nchini Tanzania, Prof. Abdallah Safari na Rais Mstaafu wa Chama cha Mawakili Tanzania (TLS), Tundu Lissu, wameshauri wajumbe wa chama hicho kumchagua Dk. Edward Hoseah, kuwa rais wao. Anaripoti Yusuph Katimba, Dar es Salaam … (endelea).

Kila mmoja kwa wakati wake wameelea, katika wagombea watano waliojitokeza kuwania nafasi hiyo, Dk. Hoseah anazo sifa zisizofikiwa na mgombea yeyote ikiwa ni pamoja na umahiri katika masuala ya sheria na uongozi nchini.

Wagombe waliochukua fomu, kurejesha na kupitishwa kugombea urais wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika tarehe 15 Aprili 2021, jijini Arusha ni; Albert Msando, Shehzada Walli, Flaviana Charles, Francis Stolla na Dk. Hosseah, aliyewahi kuwa mkurugenzi mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupamba na rushwa (Takukuru).

Akizungumza na MwanaHalisi Online leo Alhamis tarehe 7 Aprili 2021, Prof. Safari amesema, TLS inahitaji rais mwenye maono na uwezo.

“Msando anajulikana kutokana na matuhuma yake, dunia yote inajua tuhuma zake. Huyo waachane naye, lakini Stolla tayari amekuwa rais na watu wanamjua, itoshe.”

“Chama kinahitaji kiongozi mpya, tena mwenye uwezo wa kurejesha TLS kwenye mstari, nikiangalia hawa watatu waliobaki (Dk. Hoseah, Flavian ana Walli), mwenye uwezo ni Dk. Hoseah, anazo sifa zote. Mimi karata yangu inaangukia kwa Dk. Hoseah,” amesema Prof. Safari.

Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti Chadema

Akifafanua sababu za Dk. Hosea kuwa anafaa, anasema mgombea huyo amefanya kazi nyingi, na anaeleweka uwezo wake kwa watu wote akisitiza kwa wakati huu, ndio mtu anayefaa zaidi.

“Ukiachana na Dk. Hoseah, hao wengine siwajui kabisa, wangekuwa wamefanya kazi kubwa na hata kufika Mahakama ya Rufaa ninewajua, lakini siwajua kabisa. Ni wapya bado bado kidogo,” ameeleza Prof. Safari.

Lissu aliyeongoza chama hicho mwaka 2017, ameshauri wajumbe wa TLS kumchagua Dk. Hoseah, na kwamba atawasaidia kuongoza katika utawala wa sheria.

Shehzada Walli mgombea Urais TLS

Lissu ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema kwa sasa, amesema “namfahamu Hoseah kwa karibu zaidi kuliko wengine na kwa maana hiyo, siwezi kuwaunga mkono.”

“Kwa sababu namfahamu na nafahamu msimamo wake, kama mwanachama wa TLS na nafahamu msimamo wake nje ya TLS hasa kwenye masuala ya kisheria na utawala wa sheria,” amesema Lissu alipozungumza na MwanaHALISI Online kwa simu akiwa nchini Ubelgiji.

Lissu amesema, akiwa mbunge wa Singida Mashariki “nilipata fursa ya kufanya naye kazi nikiwa bungeni, yeye akiwa mkurugenzi mkuu wa Takukuru. Alikuwa anakuja na nilipata fursa ya kuelewa msimamo wake.”

“Nje ya Takukuru, nafahamu historia yake kama mwanasheria, Dk. Hoseah alikuwa msaidizi wa Jaji (Francis) Nyalali, lakini alikuja kugombana na Nyalali vibaya sana kwa sababu ya msimamo tu na ndiyo ilimfanya akaondoka mahakamani,” amesema Lissu na kuongeza:

“Katika hali ya nchi yetu, kwenye miaka mitano iliyopita, tunahitaji TLS imara na TLS imara, lazima ipate kiongozi ambaye ni imara na msimamo ambao hatakubali kuyumbishwa. Kwa sababu ni mtu ninayemfahamu, nina imani katika mazingira haya na kwa wagombea waliopo ni mgombea bora.”

Albert Msando, mgombea Urais TLS

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Zanzibar mbioni kuanza uchimbaji mafuta na gesi baharini

Spread the loveSERIKALI ya Zanzibar, imekamilisha mchakato wa uchimbaji wa mafuta na...

Habari za Siasa

Wizara ya afya yataja mafanikio 10 miaka mitatu Samia madarakani

Spread the loveWIZARA ya Afya imetaja mafanikio 10 iliyoyapata ndani ya miaka...

Habari za Siasa

Mbozi walilia kuwa manispaa, majimbo 3

Spread the loveHALMASHAURI ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe imeeleza dhamira yake...

Habari za Siasa

Wabunge waitaka TPDC kuongeza kasi ya kuunganisha wateja gesi asilia

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini...

error: Content is protected !!