February 26, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mchengerwa alia tatizo la umeme Rufiji

Fundi umeme wa Tanesco akiunganisha umeme wa REA katika moja ya nyumba zilizopo kijijini

Spread the love

MBUNGE wa Rufiji Mohammed Mchengerwa(CCM) amehoji ni lini serikali itawaunganisha wananchi wa Rufiji,Kibiti na Kilwa kwenye grid ya taifa, anaandika Dany Tibason.

Akiuliza swali jana bungeni, kwa niaba ya Mchengerwa,Mbunge wa Kilolo,Venance Mwamoto(CCM) alidai ni takribani miaka miwili sasa serikali imeshindwa kuwahakikishia wananchi wa jimbo la Rufiji kuwa na umeme wa uhakika.

“Je ni lini serikali itawaunganisha wananchi wa Rufiji, Kibiti na Kilwa kwenye Grid ya Taifa,’? aliuliza

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Dk Medard Kalemani, amesema Wilaya za Kilwa, Rufiji na Kibiti, zitaunganishwa katika gridi ya taifa kupitia utekelezaji wa mradi wa ujenzi kutoka Somanga,Fungu(Lindi) hadi Kinyerezi Dar es salaam.

“Mradi huu utaunganisha na kusafirisha umeme utakaozalishwa katika Kituo cha Somanga, Fungu kwenye uwezo wa kuzalisha MW 240,”alisema

Amesema kazi inayofanywa kwa sasa ni pamoja na kukamilisha malipo ya fidia kwa wananchi watakaopitisha mradi na kwamba kazi ya ujenzi huo inatarajiwa kuanza Julai 2018 na kukamilika Desemba 2020.

error: Content is protected !!