Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge Tarimo ataka TFDA irejeshwe
Habari za Siasa

Mbunge Tarimo ataka TFDA irejeshwe

Spread the love

Mbunge wa Moshi Mjini, Priscus Tarimo (CCM) ameitaka wizara ya afya kutekeleza mapendekezo yaliyotolewa na kamati mbalimbali za Bunge kwamba iliyokuwa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) irejeshwe kwa kuwa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeshindwa kushughulikia masuala ya chakula. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Tarimo amebainisha hayo bungeni leo Jumatatu katika maswali aliyouliza ambapo kwenye swali la msingi alihoji mpango wa serikali kurejesha TFDA kwani imeacha masuala ya chakula na inakinzana na utaratibu wa usimamizi wa chakula na madawa duniani.

Akijibu maswali hayo, Naibu Waziri wa Afya, Dk. Godwin Molel amesema suala la kurejesha usimamizi huo wa masuala ya chakula kwa TMDA bado linaendelea kujadiliwa ndani ya Serikali na mara litakapokamilika mapendekezo ya utekelezaji yatawasilishwa Bungeni.

“Serikali katika kuimarisha mazingira ya biashara nchini, ilifanya maamuzi kupitia Bunge ya kuhamisha majukumu ya usimamizi na udhibiti ubora wa chakula na vipodozi kutoka iliyokuwa TFDA na kuyapeleka TBS ambako ndiko afua zote za usimamizi zinatekelezwa huko kwa sasa,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

error: Content is protected !!