September 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge ataka gongo itumike kuikabili corona

Spread the love

PROFESA  Jumanne Kishimba, Mbunge wa Kahama (CCM), ameishauri serikali kuruhusu pombe ya gongo, itumike katika kukabiliana na mlipuko wa Virusi vya Corona, kwa wananchi wasio na uwezo wa kununua vitakasa mikono (Sanitizer). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Prof. Kishimba ametoa ushauri huo jana tarehe 6 Aprili 2020, bungeni jijini Dodoma.

Amemuomba Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, kuruhusu matumizi ya pombe hiyo kwa kuwa ina kiwango cha kilevi kinachokaribiana na kiwango cha vitakasa mikono.

“Tunamuomba waziri wa afya sasa, kwa kiwa wananchi hawawezi kununua sabuni tunazotumia ambazo zina alcohol asilimia 65, atamke kwa muda huu wa dharura wananchi wanawie gongo ili kuzuia suala la Corona,” amesema Prof. Kishimba na kuongeza:

“Mheshimiwa Spika sanitizer ina alcohol asilimia 65 na gongo ina asilimia 55, inaonekana inafaa kuliko spiriti zilizopo.”  Kwa mujibu wa serikali, Tanzania ina idadi ya wagonjwa 24 wa COVID-19.

error: Content is protected !!