Thursday , 30 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge ataka elimu bure kidato tano na sita, serikali yamjibu
Habari za Siasa

Mbunge ataka elimu bure kidato tano na sita, serikali yamjibu

Spread the love

 

BONIFACE Mwita Getere, Bunda Vijijini (CCM), ameitaka serikali kueleza, kwamba ina mpango gani wa kukamilisha dhana ya elimu bure. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

“Je serikali ina mpango gani wa kukamilisha dhana ya elimu bure kwa kutoa elimu bure kuanzia Shule ya Msingi hadi Kidato cha Tano na cha Sita,” ameuliza Getere leo tarehe 11 Februari 2021 bungeni, jijini Dodoma.

Akijibu swali hilo, Naibu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknoloji, Omary KIpanga amesema, dhana ya utoaji elimu msingi bila malipo, inamaanisha mwanafunzi atasoma bila mzazi/mlezi kulipa ada wala michango ya fedha iliyokuwa ikitozwa kabla ya kutolewa kwa Waraka wa Elimu Na. 5 wa Mwaka 2015.

“Gharama hizo zote ambazo mzazi/mlezi alitakiwa kutoa kwa sasa hulipwa na serikali. dhana ya elimu bila malipo inalenga eneo la elimumsingi.

“Elimu hii inaanzia elimu ya awali hadi elimu ya sekondari Kidato cha Nne ili kuwajengea watoto wa Kitanzania misingi imara ya masomo, ngazi zinazofuata na ustawi wa maisha yao kwa ujumla,” amesema Kipanga.

Na kwamba, elimu ya Kidato cha Tano na Sita nchini hutolewa kwa ushirikiano kati ya wazazi/walezi na serikali.

“Wazazi/walezi hutakiwa kuchangia ada ya Sh.70,000 kwa wanafunzi wa shule za bweni na Sh.20,000 kwa wanafunzi wa shule za kutwa kwa mwaka,” imeeleza wizara hiyo na kuongeza:

“Serikali hugharamia gharama nyingine zilizobaki kama vile mishahara ya walimu, vifaa vya kufundishia na kujifunzia kwa mfano vitabu na vifaa vya maabara pamoja na ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya shule.”

Kipanga amesema, katika mpango huu wa sasa, kidato cha tano na sita itatekelezwa iwapo bajeti itakaa sawa kwani hakuna shaka.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!