May 17, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mtifuano Ligi Kuu raundi ya pili

Spread the love

 

MZUNGUKO wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara utaanza kesho tarehe 11 Februari 2021, huku kukiwa na kitendawili kikubwa kwenye kumpata bingwa wa taji hilo kutokana na ushindani wa mafarasi watatu kwenye mbio hizo ambazo tamati yake itakuwa Juni mwaka huu. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Tayari mpaka sasa michezo michezo 18 imeshachezwa kwa timu 15 kati ya 18 zinazoshiriki Ligi Kuu msimu huu, huku Simba na Namungo FC wakiwa na michezo mkononi kutokana na ushiriki wao kwenye michuano ya kimataifa.

Vinara wa ligi hiyo, klabu ya Yanga wanakwenda kufungua duru la pili dhidi ya Mbeya City, huku wakiwa na rekodi ya kutofungwa mchezo hata mmoja katika mechi 18 walizocheza kwenye mzungo wa kwanza na kujikusanyia jumla ya pointi 44.

Simba ambayo ipo katika nafasi ya pili ikiwa imecheza michezo 17 ikiwa na pointi 39, ikiwa na mchezo mmoja mkoni dhidi ya Namungo FC ataanza kampeni ya kutetea ubingwa wake kwenye mzunguko wa pili dhidi ya Biashara United ya kutoka Mara tarehe 18 Februari 2021.

Nafasi ya tatu inakamatwa na Azam FC ambao mzunguko wa kwanza walianza ligi hiyo vizuri kwa kushinda michezo saba mfululizo na baadae timu hiyo ikapoteza mwelekeo kwa kutopata ushindi kwenye michezo mitano mfululizo.

Azam FC kwa sasa ina pointi 33 baada ya kucheza michezo 18, huku ikiwa nyuma ya Yanga kwa pointi 11 ambaye anaongoza Ligi hiyo na kesho itashuka dimbani dhidi ya Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga kwa mchezo wa raundi ya pili ya Ligi Kuu.

Mafarasi hao watatu waliopo juu kwenye msimamo kila mmoja ana nafasi ya kushinda ubingwa huo kwa kuwa wanavikosi imara mara baada ya kufanya nyongeza ya wachezaji kwenye usajili wa dirisha dogo lilifungulia kuanzia tarehe 15 Desemba, 2020 mpaka tarehe 15 Januari 2021.

Utamu wa mzungo wa pili hautoishia kwenye mbio za ubingwa tu, bali hata kwa timu zinazopambana kushuka daraja ambazo zipo chini ya msimamo huo.

Kwa sasa klabu kutoka Mbeya zinaonekana kuwa na hali mbaya zaidi kwa kushika nafasi mbili za chini ambapo Ihefu FC ipo nafasi ya 18, ikiwa na pointi 13 mara baada ya kucheza michezo 18, ikifuatiwa na Mbeya City kwenye nafasi ya 17 ikiwa na pointi 14 baada ya kucheza michezo 18.

Kama Mbeya City na Ihefu FC watashinda kujikwamua kwenye nafasi hizo basi zitashuka daraja moja kwa moja huku timu ambazo zitakuwa kwenye nafasi ya 15 na 15 ambapo kwa sasa wapo Mwadui FC yenye pointi 15, pamoja na Gwambina zitakwenda kucheza mtoano (Play off) na timu za daraja la kwanza.

Mpaka tunakwenda kuanza mzungko wa pili hapo kesho klabu ya Simba ndiyo timu inaongoza kwa kufunga mabao mengi ambapo mpaka sasa wamepachika jumla ya mabao 41, wakifuatiwa na Yanga waliokwamisha kambani mabao 29.

Prince Dube

Lakini pia mpaka kukamilika kwa raundi ya kwanza, Yanga ndiyo timu iliyofungwa mabao machache ambapo kwenye michezo 18 waliocheza wameruhusu mabao saba, huku Mwadui ndiyo timu iliyofungwa mabao mengi kwa kukubali nyavu zao kutikiswa mara 34 katika michezo 18 waliocheza.

Kinara wa ufunguka kwa sasa kwenye ligi hiyo ni mshambuliaji wa klabu ya Simba, Meddie Kagere aliyepachika mabao 9, huku akifuatiwa na John Bocco mwenye mabao nane na nafasi ya tatu inashikwa na Adam Adam kutoka JKT Tanzania mwenye mabao saba, sawa na Prince Dube wa Azam FC.

Rekodi nzuri ya Simba kwenye mzunguko wa kwanza haikushia kutoa wafungaji bora pamoja na kufunga mabo mengi, katika michezo yote ya mzunguko wa kwanza kiungo wa Simba, Clatous Chama ndiye mchezaji aliyepiga pasi nyingi zilizozaa mabao (assist) kwa kufanya hivyo mara tisa.

Nafasi ya pili ikishimwa tena na kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba, Luis Miquison aliyepiga pasi nane, huku nafasi ya tatu ikishikwa na Price Dube kutoa Azam FC mwenye pasi sita.

Raundi hiyo ya pili itaanza kesho kwa kupigwa michezo mitatu ambapo Azam FC itakuwa ugenini kwenye dimba la Mkwakwani kuwakabili Coastal Union, huku Kagera Sugar wataalika Gwambina kwenye Uwanja wa Kaitaba.

error: Content is protected !!