May 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Askofu Ruwa’ichi amlilia Padri Boyo

Marehemu Padri Ernest Donald Boyo, aliyekuwa Paroko Msaidizi wa Parokia ya Chang'ombe

Spread the love

PAROKO Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Parokia ya Chang’ombe, Padri Ernest Donald Boyo, amefariki dunia usiku wa jana Jumatano tarehe 10 Februari 2021. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa ya kifo cha Padri Boyo imetolewa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Jude Thaddaeus Ruwa’ichi.

Askofu Riwa’ichi amesema, Padri Boyo amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dar es Salaam alikokuwa anapatiwa matibabu.

“Kwa masikitiko makubwa napenda kuwataarifu juu ya kifo cha Padri wetu mpendwa Boyo wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, aliyekuwa Paroko Msaidizi wa Parokia ya Chang’ombe.”

Yuda Thaddaeus Ruwa’ichi, Askofu Mkuu Mwandamizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam

“Padri Boyo amefariki leo (jana), tarehe 10 Februari 2021 saa 1:30 usiku katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili alipokuwa akitibiwa,” amesema Askofu Ruwa’ichi.

Askofu Ruwa’ichi amesema taarifa za mazishi ya mwili wa Padri Boyo zitatolewa baadae baada ya taratibu hizo kukamilika.

“Taarifa zaidi juu ya taratibu za Mazishi zinapangwa na tutawataarifu. Tumuombee Pumziko la Milele Mbinguni,” amesema Askofu Ruwa’ichi.

error: Content is protected !!