Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe: ICC haitawaacha
Habari za Siasa

Mbowe: ICC haitawaacha

Spread the love

FREEMAN Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amesema vyombo vya ulinzi na usalama vinavyokiuka haki, hata kama vikilindwa na serikali ya Tanzania, havina kinga katika jumuiya za kimataifa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza na wanahabari leo tarehe 16 Machi 2020, jijini Dar es Salaam, amewaeleza viongozi hao amesema “niwaambie viongozi wa majeshi wanaotumia nguvu wasidhani wana kinga duniani.

“Wasidhani wana kinga ya serikali, wajue hawana kinga katika jumuiya za kimataifa. Watambue kuna Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC). Haya mambo ya kutumia ofisi kulinda masilahi ya watu wakitumia ofisi zao kubagua watu, ipo siku watawajibika.”

Mbowe ameeleza hayo wakati akizungumzia madhila waliyokutana nayo baadhi ya viongozi wa Chadema, waliokwenda kumtoa katika Gereza la Segerea jijini Dar es Salaam.

“Iwavyo vyovyote matumizi ya nguvu za ziada za kupiga, kutesa na kujeruhi wanawake haviwezi kukubalika mbele ya jumuiya yoyote katika dunia hii. Bila kujali sheria gani inazungumza na mazingira gani,” amesema Mbowe na kuongeza:

“Wanavunja mbunge mkono wakisema waliowachangia wakalipie huduma ya kutibu mkono, wanapigwa wakuu viongozi wa magereza wapo wanashuhudia . Hilo jambo tunalilaani kwa nguvu zote.

“Hawakua na fimbo wanapigwa na wanaume, risasi zinapigwa za moto. Wanapambana na Halima Mdee, Esther Bulaya na  Jesca Kishoa, hawa ni wa mama. Hata katika sheria za magereza wanaoruhusiwa kushuhulika na wanawake ni wanawake tu.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!