Sunday , 19 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mbinu za kumuenzi Nyerere kiuchumi zaainishwa
Habari Mchanganyiko

Mbinu za kumuenzi Nyerere kiuchumi zaainishwa

Spread the love

SERIKALI imesema inaendelea kutekeleza mikakati itakayosaidia kutimiza ndoto za Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere ili kuimarisha ustawi wa wananchi na maendeleo ya uchumi. Anaripoti Regina Mkonde… (endelea).

Hayo yameelezwa jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Francis Michael, akifungua kongamano la kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, lililofanyika Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Kongamano hilo linalofanyika siku mbili, Jumanne na Jumatano, ya tarehe 12 Oktoba 2022, lenye kauli mbiu ya ‘mchango wa Mwalimu Nyerere katika uimarishaji ustawi wa watu na maendeleo ya uchumi wa kijamii’, limeandaliwa na Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA).

Dk. Michael alisema Rais Samia Suluhu Hassan anapita katika njia za Mwalimu Nyerere, Kwa kuhakikisha mfumo wa elimu unabadilika na kuwa tegemezi.

“Ukiangalia mageuzi ambayo Rais Samia anayasimamia, kwamba anaendelea kupita kwenye hatua zilezile ambazo Baba wa Taifa alikuwa anapita. Nyerere alisistiza watu wapate elimu ya kujitegemea iliyokuwa na lengo mahususi ya kwamba watu wanapomaliza elimu katika daraja lolote aweze kupata uzoefu na ubobevu wa kujiajiri,” alisema Dk. Michael.

Dk. Michael alisema, ili kufanikisha mageuzi hayo, Serikali inakamilisha mchakato wa maboresho ya sekta ya elimu, ikiwemo kufumua mfumo wake na mitaala, huku akitoa wito kwa wananchi kutoa maoni yao kuhusu zoezi hilo wakati utakapofika.

Aidha, Dk. Michael ameupongeza uongozi wa chuo Cha MNMA kwa kuandaa kongamano hilo lenye mada nne, zenye lengo la kutoa suluhu ya maadui watatu waliopigwa vita na Mwalimu Nyerere, ujinga, umasikini na maradhi.

Naye Mkuu wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Profesa Shadrack Mwakalila, alisema wameandaa komgamano hilo ili kuenzi mchango wa Mwalimu Nyerere, katika kupambana naaadui hao.

“Moja ya jambo ambalo tumeona kongamano hili tuweze kulifanya maalum katika suala la kupambana na maadui watatu wa maendeleo ambao mpaka sasa tunapambana nao hatujafanikiwa kuwashinda kwa asilimia 100. Ni wajibu wetu kuhakikisha tunasaidia jamii kwa ujumla kupambana nao tunapotoa mafunzo na kuandaa makongamano,” alisema Prof. Mwakalila.

Prof. Mwakalila alisema katika kongamano hilo washiriki watajadili tafiti takribani 30, zilizofanywa na wanataaluma kutoka sehemu mbalimbali, ambazo zimebeba majibu juu ya changamoto zinazoikabili jamii.

Mtoa mada katika kongamano hilo, Dk. Bertha Mleke, ameishauri Serikali iwahimize vijana kusoma maandiko ya Mwalimu Nyerere, ili waweze kuyaishi.

“Mfano ukiwa nchi za watu wanamuenzi Mwalimu Myerere, nasi tuzingatie mawazo yake sababu yanaishi hususan kwenye walimu amesisitiza sana elimu ya kujitegemea. Mawazo yake bado yanaishi na Serikali itizame kwa jicho la ziada kuwasisitiza vijana kusoma nyaraka zake. Pia iboreshe elimu kupitia mawazo yake kwani yamegusa kila mtu,” alisema Dk. Mleke.

Kwa upanda wake, Dk. Philip Daninga, ambaye pia ni Mhadhiri wa Uchumi katika chuo hicho, ameishauri Serikali iwajengee uwezo wananchi kuhusu masuala ya viwanda ili kuongeza ushiriki wao katika sekta hiyo.

Alisema suala hilo likifanyika kikamlifu, litasaidia kuenzi ndoto za Mwalimu Nyerere katika kujenga uchumi wa viwanda.

“Mwalimu Nyerere alifanya kazi kubwa kuanzisha viwamda, alianzisha vingi lakini bado tunahangaika na viwanda. Rais wa sasa bado anasisitiza viwanda. Tuwajengee uelewa wananchi kuhusu viwanda sababu tumeacha kuwashirikisha. Sera ya viwanda wananchi wakiielewa watashiriki. Mfano tuna rasilimali nyingi lakini hukuti watu wakishiriki kuanzisha viwanda vidogo,” alisema Dk. Daninga.

Miongoni mwa mada zinazojadiliwa katika kongamano hilo, ni umasikini adui wa maendeleo ya uchumi wa kijamii, udhibiti wa magonjwa kwa uimarishaji wa ustawi wa watu na uongozi na utawala bora katika mapambano dhidi ya ujinga, umasikini na maradhi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Canada yatenga bilioni 38 kutekeleza mradi ya kuinua vijana TZ

Spread the loveSERIKALI ya Canada kupitia ‘CARE International Canada’ imetenga takribani Sh...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Ujenzi kituo cha kupoza umeme Chalinze wafikia asilimia 93.7

Spread the loveKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeeleza...

Habari Mchanganyiko

Balile ateuliwa rais wa wahariri Afrika Mashariki

Spread the loveJumuiya ya Wahariri wa Afrika Mashariki (EAES), imemchagua Mwenyekiti wa...

error: Content is protected !!