Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbatia aitaka Serikali itoke mafichoni mgawo wa maji, wamachinga
Habari za SiasaTangulizi

Mbatia aitaka Serikali itoke mafichoni mgawo wa maji, wamachinga

James Mbatia, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi
Spread the love

 

MWENYEKITI wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, ameiomba Serikali itoke hadharani, ili itoe majibu dhidi ya changamoto za mgawo maji na sakata la wamachinga. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mbatia ametoa wito huo leo Jumamosi, tarehe 13 Novemba 2021 akihutubia katika mkutano wa Kamati Kuu ya NCCR-Mageuzi, uliofanyika jijini Dar es Salaam.

“Leo hii mnatuambia Jiji la Dar es Salaam, halina maji hata Serikali haielezi sababu gani? hakuna sababu ya msingi. Eti vyanzo vya maji Ruvu vimekauka, eti kuna mgawo wa maji halafu Watanzania ni kimya tu,” amesema Mbatia.

Mwenyekiti huyo wa NCCR-Mageuzi amesema kuwa, changamoto ya uhaba wa maji katika Jiji la Dar es Salaam, linatokana na Serikali kutofanyia kazi ushauri wa wapinzani juu ya namna bora ya kuvuna na kuhifadhi maji.

“Hapa tatizo la maji ni la kutisha, katikati ya jiji watu hawalali wanaamka saa sita za usiku kukinga ndoo tatu za maji, Serikali haijatuambia kwa nini na hakuna mtu kujitokeza kusema ni ukame, hapana hii ni mambo ya kiburi kudharauliana,” amesema Mbatia.

Mbatia amesema “ hoja ya namna bora ya kuhifadhi na kuvuna maji ya mvua iko nendeni mkasome hansard ya bunge ya 1996/1997 ya Mama Edith Sarafina Rusina, aliwahi kuwa makamu mwenyekiti wetu, alitoa elimu na namna bora ya kuvuna maji lakini mlisema huyu mpinzani wekeni pembeni.”

Wakati huo huo, Mbatia ameishauri Serikali iachane na njia za kuzalisha umeme kupitia vyanzo vya maji, bali itafute namna bora ya kuongeza uzalishaji wake, ili kusiwe na mgawo wa nishati hiyo.

“Umeme gani wa hydro duniani leo kweli? Lakini umeme sasa hivi tuko gizani, walisema umeme hadi kwenye vijumba vidogo kila mahali. Leo hawajatueleza mgao wa umeme umetokana na nini?” amesema Mbatia.

Changamoto ya mgawo wa maji ilitangazwa hivi karibuni na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), ambapo ilitaja chanzo chake kuwa ni kupunguwa kwa kiwango cha uzalishaji wake katika Mto Ruvu.

Akizungumzia sakata la wamachinga kuondolewa katika maeneo yasiyo rasmi, Mbatia ameishauri Serikali izungumze nao ili kupata suluhu kwa ajili ya kulinda vibarua vyao.

“Badala ya kuwapa majibu mbadala, kuwashirikisha na kuona namna ya kuwapatia ajira zinazostahili, mnawafukuza, hakuna mtu asiye fanya makosa hata NCCR-Mageuzi tumefanya makosa tumeomba radhi, kujikwaa sio kuanguka unanyanyuka na unakiri kosa,” amesema Mbatia.

Mwanasiasa huyo ameishauri Serikali itoe elimu kwa vijana itakayowasaidia kutumia rasilimali zilizopo kujiajiri, ikiwemo ya uvuvi baharini na kilimo.

“Hebu tujiulize elimu wanayopata inaweza kuwasaidia kujiajiri? Kufanya kwa vitendo kweny kilimo? Wakaenda ukanda wa bahari yetu Mungu ametujaalia,” amesema Mbatia na kuongeza:

“Eneo la bahari yetu karibu na nchi ya Uganda, tunatumiaje utajiri huu ili vijana wetu wawe kwenye uvuvi na mifugo yetu, elimu inamuandaaje kijana kuzalisha kwenye nchi yetu.”

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!