Tuesday , 23 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa MIAKA 60 UHURU: Shibuda atema nyongo hali ya kisiasa Tanzania
Habari za SiasaTangulizi

MIAKA 60 UHURU: Shibuda atema nyongo hali ya kisiasa Tanzania

Spread the love

 

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania, John Shibuda amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan aimarishe hali ya kisiasa na kidemokrasia nchini, badala ya kusubiri uchumi wa nchi uimarike kama alivyoahidi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Shibuda ametoa wito huo leo Jumamosi, tarehe 13 Novemba 2021, akihutubia katika kikao cha Kamati Kuu ya Chama cha NCCR-Mageuzi, jijini Dar es Salaam.

Mwanasiasa huyo alikuwa anazungumzia miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika, inayotarajiwa kuadhimishwa tarehe 9 Disemba 2021.

“CCM (Chama Cha Mapinduzi) na Serikali, naikumbusha duniani kote hakuna tiba ya ajali ya kuondoa na kufuta umasikini. Kwa hiyo subira ya kiungo cha uchumi kusema mpaka upevuke na ukomae, ndiyo ruksa ya siasa huru itendeke na ruksa ya demokrasia huru iruhusike, hiki ni kitendawili,” amesema Shibuda.

Kauli ya Rais Samia ya kuomba muda zaidi wa kuimarisha uchumi, aliitoa wakati akiwajibu baadhi ya Watanzania, ikiwemo wanasiasa na wanaharakati, wanaodai katiba mpya na mikutano ya kisiasa.

Makundi hayo yalipaza sauti zao kumuomba Rais Samia, atimize mchakato wa upatikanaji katiba mpya, ili kuondoa changamoto zilizopo katika medani za kisiasa na demokrasia.

Hata hivyo, Shibuda aliipinga kauli hiyo akidai kuwa, inadhulumu haki ya waasisi wa Tanzania, Baba wa Taifa, Julius Nyerere na Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Abeid Amani Karume.

“Hata Marekani wana uhuru zaidi ya miaka 200, hawajafuta umasikini, sisi Tanzania ukisema Watanzania wasubiri milango ya uchumi ikomae na kupevuka huo msimu utakuja lini?”

“ Na kupevuka lini? hicho kitendo ni cha kudhulumu heshima ya waasisi wa taifa hili, ni kumbeza Mwalimu Nyerere na Karume ambao walisema Zanzibar itakuwa nchi ya usawa, maridhiano na haki, huku kwetu demokrasia imetamkwa kila sehemu mpaka kwenye Katiba,” amesema Shibuda.

Akizungumzia hali ya kisiasa nchini, Shibuda amesema Tanzania iko katika bonde la giza.

“Hali ya kisiasa Tanzania ipo katika bonde la giza kuu, ambalo limemeza haki za Katiba na sheria kwa uhuru wa siasa na uhuru wa kidemokrasia,” amesema Shibuda.

James Mbatia, Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi

Mwanasiasa huyo mkongwe nchini Tanzania, amevitaka vyama vya siasa vijitambue na kuanza kutafuta suluhu ya changamoto inazozikabili.

Huku akiwataka wazee walioitumikia nchi, wasikae kimya dhidi ya changamoto zinazojitokeza nchini.

“Wazee wote waliotumika ndani ya nchi, wenye dhamana ya kuheshimika kwa nini wanakaa kimya? Wanajitafutia dhambi, wanakaa kimya halafu inakuwa kitanzi kwa haki za kizazi kipya,” amesema Shibuda.

Akizungumzia miaka 60 ya uhuru, Shibuda amedai Tanzania ina simanzi juu ya ukosefu wa haki ya siasa na demokrasia huru.

“Tunasherehekea miaka 60 ya uhuru, lakini tuna simanzi kwamba uhuru tunaosherehekea uliahidi Tanzania itakuwa ni ya demokrasia, lakini tuna simanzi ya kutokuwa na haki ya siasa huru na demokrasia huria,” amesema Shibuda na kuongeza:

“ Tunasherehekea tukiwa na tabasamu bandia za kufunika huzuni zetu.”

Miongoni mwa malalamiko ya vyama vya siasa, ni dosari zilizomo katika Katiba pamoja na zuio la mikutano ya vyama vya siasa, ambapo wanaoruhusiwa kufanya mikutano hiyo ni wabunge katika maeneo yao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aridhishwa utendaji mabalozi, awapa neno

Spread the loveRais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amewapongeza mabalozi  wanaowakilisha ...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mbunge ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the loveMBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze kasi...

error: Content is protected !!