Sunday , 3 December 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Matokeo kidato cha sita haya hapa
ElimuTangulizi

Matokeo kidato cha sita haya hapa

Dk. Charles Msonde
Spread the love

BARAZA la Mitihani la Taifa (Necta) nchini Tanzania, limesema watahiniwa 82,440 sawa na asilimia 98.35 ya watahiniwa 84,212 waliofanya mtihani kidato cha sita Juni/Julai 2020 wamefaulu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea)

Akitangaza matokeo hayo visiwani Zanzibar leo Ijumaa tarehe 21 Agosti 2020, Katibu Mtendaji wa Necta, Dk. Charles Msonde amesema, watahiniwa 85,499 walisajiliwa kufanya mtihani huo.

Amesema, kati yao wasichana walikuwa 36,168 sawa na asilimia 42.30 na wavulana walikuwa 49,331 sawa na asilimia 57.70.

Dk. Msonde amesema, kati ya watahiniwa waliosajiliwa, watahiniwa wa shule walikuwa 74,753 na watahiniwa wa kujitegemea walikuwa 10,746.

Amesema, kati ya watahiniwa 85,499 waliosajiliwa kufanya mtihani huo, watahiniwa 84,212 sawa na asilimia 98.49 walifanya mtihani na 1,287 sawa na asilimia 1.51 hawakufanya mtihani huo kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo ugonjwa na utoro.

Katibu mtendaji huyo amesema, watahiniwa wa shule, kati ya 74,753 waliosajiliwa, watahiniwa 74,284 sawa na asilimia 99.37 walifanya mtihani ambapo wasichana walikuwa 32,403 sawa na asilimia 99.60 na wavulana 41,881 sawa na asilimia 99.19.

Amesema watahiniwa 469 sawa na asilimia hawakufanya mtihani.

 

Kuhusu watahiniwa wa kujitegemea, Dk. Msonde amesema, watahiniwa 10,746 walisajiliwa, watahiniwa 9,928 sawa na asilimia 92.39 walifanya mtihani na 818 sawa na asilimia 7.61 hawakufanya mtihani.

“Jumla ya watahiniwa 82,440 sawa na asilimia 98.35 ya watahiniwa waliofanya mtihani wa kidato cha sita wamefaulu.”

“Wasichana waliofaulu ni 35,486 sawa na asilimia 99.07 wakati wavulana waliofaulu ni 46,954 sawa na asilimia 97.81,” amesema Dk. Msonde.

Amesema, mwaka 2019, watahiniwa waliofaulu walikuwa 88,069 sawa na asilimia 98.32.

Kuhusu ubora wa ufaulu, Dk. Msonde amesema, madaraja waliyopata watahiniwa wa shule unaonyesha jumla ya watahiniwa 72,230 sawa na asilimia 97.74 wamefaulu kati ya darala la kwanza hadi la tatu wakiwemo wasichana 31,786 sawa na asilimia 98.24 na wavulana 40,444 sawa na asilimia 97.35.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

20 wafariki dunia kwa mafuriko Manyara

Spread the loveMVUA za vuli zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini zimeleta madhara...

ElimuHabari Mchanganyiko

CEO NMB awataka vijana kunoa ujuzi wao

Spread the loveAfisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, amewashauri...

Elimu

150 wahitimu Shahada ya Udaktari HKMU

Spread the loveCHUO Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), kimeiomba serikali...

Elimu

Aliyehitimu udaktari HKMU na miaka 21 atoa siri

Spread the love MHITIMU wa fani ya udaktari ambaye ni mdogo kuwahi...

error: Content is protected !!