May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Manchester United kuivaa AC Milani, 16 bora Europa

Spread the love

 

KLABU ya Manchester United itavaana na AC Milan kwenye hatua ya 16 ya michuano ya Kombe la Europa baada ya kuchezeshwa kwa droo mchana wa leo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Kwenye mchezo wa kwanza Manchester United ataanzia nyumbani kwenye Uwanja wa Old Trafford kwa kuikalika AC Milan mchezo utakaopigwa tarehe 11 Machi 2021, na marudiano yatapigwa 18 Machi 2021, jijini Milan nchini Italia.

Timu hizo zimekutana mara 10 kwenye michezo ya kimashindano huku Manchester United ikifanikiwa kushinda michezo mitano na AC Milan ikishinda michezo mitano huku kukiwa hamna sare hata moja.

Mara ya mwisho timu hizo zilikutana kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya tarehe 10 Machi 2010, Old Trafford na Manchester United ikafanikiwa kuondoka na ushindi wa mabao 4-0.

Michezo mingine ya Europa Ligi itakayopigwa tarehe 11 Machi 2021 ni Ajax dhidi ya Young Boys, Dynamo Kyiv watawaalika Vilarreal, Roma dhidi ya Shakhtar Donestsk, Olympiacos kuikabiri Arsenal.

Pia Dinamo Zagreb wataikabili Totenham, Slavia Praha dhidi ya Rangers na Granada akiwa nyumbani ataikabiri Molde.  

error: Content is protected !!